Tanzania yapewa miji mitatu kuandaa AFCON 2027
Muktasari:
- Idadi ya timu tisa za taifa hadi sasa zimejihakikishia tiketi ya kushiriki fainali hizo ambazo ni Kenya, Tanzania, Uganda, Morocco, Senegal, Burkina Faso, Cameroon, Benin na Mali.
Tanzania imepata bahati ya miji mitatu kupewa fursa ya kuandaa mechi za Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limetangaza miji hiyo ni Dar es Salaam, Zanzibar na Arusha.
Kiujumla idadi ya miji sita itaandaa mechi za mashindano hayo ambayo yataandaliwa kwa pamoja na nchi tatu za Tanzania, Kenya na Uganda.
Kenya imepewa jiji moja tu la kuandaa mechi za mashindano hayo ambalo ni Nairobi huku Uganda yakipitishwa majiji ya Kampala na Hoima.
Fainali za AFCON 2027 zimepangwa kufanyika kuanzia Juni 19 hadi Julai 17, 2027.
Idadi ya timu tisa za taifa hadi sasa zimejihakikishia tiketi ya kushiriki fainali hizo ambazo ni Kenya, Tanzania, Uganda, Morocco, Senegal, Burkina Faso, Cameroon, Benin na Mali.
VYAMA KUOGA MANOTI
Katika hatua nyingine, Mkutano Mkuu wa CAF uliofanyika Abuja, Nigeria leo Jumamosi, Novemba 21, 2026 umetangaziwa ongezeko la fedha za uwezeshaji kwa vyama na mashirikisho wanachama wq CAF.
Kuanzia sasa, kila shirikisho na chama mwanachama wa CAF kitakuwa kikipokea kiasi cha Dola 700,000 (Sh1.9 bilioni) kwa mwaka.
Awali CAF ilikuwa ikitoa kiasi cha Dola 500,000 (Sh1.3 bilioni) kwa mwaka.