Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bursa yafungua mlango wa kumuuza Iheanacho kwa ofa nono

IHENACHO Pict

Muktasari:

  • Rais wa Bursaspor, Enes Çelik, amesema licha ya mashabiki wengi kutaka mshambuliaji huyo abaki, uongozi wa klabu hautafanya uamuzi kwa kuongozwa na hisia pekee, bali utazingatia maslahi ya timu.

ISTANBUL, UTURUKI: Klabu ya Bursaspor ya Uturuki iko tayari kumuuza mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria, Kelechi Iheanacho, iwapo itapokea ofa kubwa ya fedha, huku Fenerbahçe ikiwa miongoni mwa timu zinazomfuatilia.

Rais wa Bursaspor, Enes Çelik, amesema licha ya mashabiki wengi kutaka mshambuliaji huyo abaki, uongozi wa klabu hautafanya uamuzi kwa kuongozwa na hisia pekee, bali utazingatia maslahi ya timu.

Celik amekiri kuwa takribani asilimia 99 ya mashabiki wangepinga kuuzwa kwa Iheanacho (30), kutokana na mchango wake mkubwa tangu alipojiunga na timu hiyo.

Mshambuliaji huyo amekuwa na mwanzo mzuri Bursaspor, akifunga mabao 16 katika mechi zake 13 za kwanza na kufunga katika michezo 12 kati yake, akiiongoza timu hiyo katika harakati za kupanda daraja kwenda Ligi Kuu ya Uturuki.

Akizungumza na chombo cha habari cha Turkinform, Celik alisema angependa zaidi Iheanacho aendelee kubaki kikosini, lakini ofa kubwa isiyo ya kawaida italazimisha uongozi kutathmini uwezekano wa kumuuza.

IHEN 01

“Najua asilimia 99 ya mashabiki wangu kusema hapaswi kuuzwa kabisa. Ninaelewa hilo, lakini hatuwezi kuangalia suala hili kwa hisia pekee. Tunapaswa pia kulitathmini kwa mantiki,” alisema.

Aliongeza: “Ningependa Iheanacho abaki kwenye timu kuliko mtu mwingine yeyote. Lakini huenda kukawa na ofa kubwa sana za fedha. Zikitolewa, sisi kama uongozi tutazipitia na hatimaye kufanya kile tunachoona ni sahihi kwa klabu.”

Wakati huo huo, Iheanacho anatarajia kujumuishwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria kitakachokabiliana na Tanzania katika michezo miwili ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 mwezi huu wa Novemba.