Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Basi la Leicester City litaishia wapi safari hii?

Muktasari:

Katika kikosi chao cha sasa Leicester imebakisha wachezaji wawili tu wanaocheza mara zote kutokea katika kikosi cha bingwa. Jamie Vardy na kipa, Kasper Schmeichel. Hauwezi kusema hawastahili kuwepo kikosini. Kule mbele Vardy ni moto na ndiye mfungaji bora wa Ligi Kuu mpaka sasa. Kule nyuma, Schmeichel bado ni moto.

HATUJUI basi la Leicester City litaishia wapi safari hii. Kitu cha msingi ni kwamba wanatutia hofu. Miaka sita iliyopita wasingetutia hofu lakini kwa sasa wanatutia hofu.

Kwanza kabisa tunakumbuka mwendo wao mdundo wa msimu wa 2015/16. Ilianzia kama masihara wakachukua ubingwa. Tuna lile jinamizi. Hatuwaamini tena. Hatuwadharau tena. Wana kitu cha kutukumbusha mkononi.

Hii ndio maana halisi ya jinamizi. Kuna wakati linakuganda kupita kiasi. Na sasa Leicester wamerudi tena kutuganda katika jinamizi. Wanacheza soka la uhakika. Hawabahatishi katika ushindi wao. Wana kocha ambaye amewafanya wacheze soka la uhakika, Brenda Rodgers.

Katika kikosi chao cha sasa Leicester imebakisha wachezaji wawili tu wanaocheza mara zote kutokea katika kikosi cha bingwa. Jamie Vardy na kipa, Kasper Schmeichel. Hauwezi kusema hawastahili kuwepo kikosini. Kule mbele Vardy ni moto na ndiye mfungaji bora wa Ligi Kuu mpaka sasa. Kule nyuma, Schmeichel bado ni moto.

Maeneo mengine ambayo wamebadili kikosi chote, Leicester wametimia. Walinzi wao wa pembeni, Ricardo Perreira kulia ni moto, na Ben Chilwell kushoto ni moto mkali. Walinzi wao wa kati, Caglar Soyuncu ni moto wakati Jonny Evans amezaliwa upya.

Katika kiungo wana watu watatu. Wilfried Ndidi anasimama nyuma ya viungo wawili wasambazaji ambao ni hatari kwa pasi za mwisho. Muingereza James Maddison na Mbelgiji Youri Tielemans. Ndidi kazi yake ni kulinda ukuta na kuwapasia Maddison na Tielemans ambao ni watu hatari katika kutengeneza mashambulizi. Mbele, Leicester wana Vardy lakini pia wana Ayoze Perez ambaye ana kazi mbili. Anaweza kuwasaidia akina Maddison lakini pia anaweza kufunga. Kuna Kelechi Ihenacho pia. Usishangae kuona Southampton wakipigwa mabao 9-0 nyumbani.

Hatujui safari hii basi la Leicester litafika wapi lakini kwa mara nyingine wana timu bora kuliko Manchester United, Chelsea, Arsenal na Tottenham. Nawaona wakienda Top Four. Siwaoni Leicester hawa wakipoteza mechi tatu mfululizo.

Na katika ubingwa, kikwazo chao pekee msimu huu kinaweza kuwa kitu kimoja tu. Timu moja tu. Liverpool, basi.