Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bubista apewa kazi RS Berkane

Muktasari:

  • Baada ya kuitumikia Cape Verde kwa mafanikio kwa kipindi cha miaka sita na kuiwezesha timu hiyo kufuzu hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia 2026 kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo.

RABAT, Morocco: BAADA ya kujiuzulu kuifundisha timu ya taifa ya Cape Verde, Bubista amepewa kibarua kizito cha kuwanoa mabingwa wa Morocco, RS Berkane.

Baada ya kuitumikia Cape Verde kwa mafanikio kwa kipindi cha miaka sita na kuiwezesha timu hiyo kufuzu hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia 2026 kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo.

Cape Verde ilifika hatua ya 32 bora kabla ya kutolewa kwa kufungwa mabao 3-2 katika muda wa ziada dhidi ya Argentina, ambao baadaye walimaliza mashindano hayo wakiwa washindi wa pili.

Bubista pia aliiongoza Cape Verde kufika hatua ya robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023, mafanikio yaliyomfanya kuwa miongoni mwa makocha waliofanikisha makubwa katika historia ya soka la taifa hilo.

Baada ya kuondoka katika kikosi hicho, Bubista amesaini mkataba wa miaka miwili na RS Berkane, akichukua nafasi ya Moin Chaabani ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Tunisia.

Shirikisho la Soka la Cape Verde limemshukuru Bubista kwa kujitolea kwake na mchango alioutoa katika kuendeleza timu ya taifa, huku likimtakia mafanikio katika hatua inayofuata ya maisha yake ya ukocha.

Uteuzi huo unampeleka Bubista katika moja ya klabu zinazoongoza barani Afrika. RS Berkane ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu Morocco msimu uliopita na imekuwa ikishiriki mara kwa mara katika mashindano ya klabu yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).