Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bruno akataa Sh725 Bilioni

Muktasari:

  • Mchezaji huyo anadaiwa kwamba alipewa ofa ya mkataba wa miaka mitatu ambao ungemwezesha kukunja Pauni 200 milioni kama mshahara ambayo haikuwa inakatwa kodi, lakini amekataa kwenda kujiunga na Saudi Pro League.

MANCHESTER, ENGLAND: SUPASTAA wa Manchester United na timu ya taifa ya Ureno, Bruno Fernandes amekataa ofa ya kushangaza kutoka Al-Hilal ya Saudi Arabia.

Mchezaji huyo anadaiwa kwamba alipewa ofa ya mkataba wa miaka mitatu ambao ungemwezesha kukunja Pauni 200 milioni kama mshahara ambayo haikuwa inakatwa kodi, lakini amekataa kwenda kujiunga na Saudi Pro League.

Taarifa za mchezaji kuwa anaweza kuondoka Man United zimekuwa sio habari tena kwani hata yeye yupo tayari kufanya hivyo. Fernandes, mwenye umri wa miaka 30, alikuwa Asia wiki iliyopita kwenye ziara ya Man United baada ya msimu kumalizika na wakati huohuo, wakala wake Miguel Pinho alienda Riyadh kwa mazungumzo na viongozi wa Al-Hilal.

Timu hiyo ya Ligi Kuu ya Saudi Arabia ilikuwa inataka jibu la haraka kabla ya kushiriki Kombe la Dunia la Klabu ikiwa Bruno anataka kujiunga nayo au la.

Kwa mujibu wa mtaalamu wa usajili Ulaya, Fabrizio Romano, nyota huyo ameamua kuikataa Al-Hilal kwa sababu anataka kuendelea kucheza soka la ushindani Ulaya.

Fernandes kwa sasa ana mkataba na kuitumikia Man United hadi majira ya kiangazi 2027 na vigogo wa timu hiyo wana chaguo la kuuongeza kwa mwaka mmoja zaidi ikiwa watataka.

Kwa mujibu wa Ben Jacobs, Fernandes alikataa ofa ya Al-Hilal baada ya kujadiliana na familia yake.

Kiungo huyo mshambuliaji pia alionekana akila chakula cha jioni na mchezaji wa Al-Hilal na timu ya taifa ya Ureno, Joao Cancelo.

Baada ya United kufungwa kwenye fainali ya Europa League na Tottenham Hotspur, Fernandes alifungua mlango wa uwezekano wa kuondoka klabuni ambapo akisema: “Nimekuwa mkweli kila wakati. Nimesema kila mara nitakuwa hapa hadi pale klabu itakaponiambia kuwa muda wa kuondoka umefika. Nina hamu ya kufanya zaidi, kuweza kuirudisha timu kwenye zama zake. Nitaondoka siku ambayo klabu itafikiri kuwa mimi ni mzigo au muda umefika wa kuachana, mpira uko hivyo, hujui lini. Lakini nimesema mara nyingi na ninasimamia maneno yangu.”

Baadaye Fernandes alicheza katika mechi ya mwisho ya msimu ambapo Man United ilishinda dhidi ya Aston Villa pamoja na michezo yote miwili ya kirafiki baada ya msimu.

Alipoulizwa ikiwa nahodha wake ataondoka, kocha Ruben Amorim alisema: “Sidhani kama ni hivyo sijui kwa uhakika. Hakuna anayejua, lakini sidhani kama ni hivyo. Anaona tunafanya mabadiliko fulani na nafikiri hicho ndicho anachotaka ili abaki. Ni kijana sana, ni mzuri sana. Anahitaji kuwa kwenye ligi bora zaidi duniani.”