Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hatimaye wakubwa wamepakimbia Uhuru

WAKUBWA Pict

Muktasari:

  • Hizi timu mbili za Kariakoo washkaji zangu tuliyasema haya kwamba ni vigumu kutumia kwa pamoja uwanja ule.

LILIKUWA suala la muda tu na hata hapa kijiweni tulishawahi kulitabiri hili la kuukacha Uwanja wa Uhuru.

Hizi timu mbili za Kariakoo washkaji zangu tuliyasema haya kwamba ni vigumu kutumia kwa pamoja uwanja ule.

Tulipoona ratiba ya ligi imetoka, mimi na wanangu hapa tuliamini kwamba pale patakimbiwa.

Mechi mbili tu zimetosha kuwafanya jamaa wapachoke pale na wote wameshachagua viwanja vingine watakavyovitumia msimu huu.

Baada ya kufungwa na Wakongo tu, ghafla tukaona mainfluensa wa Yanga baadhi wakiutaka uongozi wao uondoke pale Uhuru eti wanasema mazingira sio rafiki.

Hatimaye wanetu wamekuja hapo jirani tu na maskani yetu, katika Uwanja wa KMC hapo Mwenge ambao waliutumia msimu uliopita.

Haya Simba nao wamekula mtaa kwa kupaacha Uwanja wa Uhuru na wamerudi katika Uwanja wa Isamuhyo kule Mbweni kwa mechi zao za nyumbani.

Tungesema hili jambo tulibetie si leo hapa kijiweni wanangu tungepata hela kimtindo maana limetimia sana kabla hata hapajachezwa mechi ya ligi.

Wameishia kuutambulisha Uhuru katika matamasha yao lakini katika matumizi wameuacha wameuacha kwenye mataa.