Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nuno Espirito ‘kuliwa kichwa’ West Ham United

NUNO Pict

Muktasari:

  • Kocha huyo raia wa Ureno mwenye umri wa miaka 52, kwa sasa yupo kwenye mazungumzo na bodi ya klabu hiyo baada ya safari ya miaka 14 ya West Ham kwenye ligi hiyo kuhitimishwa katika mchezo wa mwisho wa msimu jana, Jumapili, Mei 24, 2026.

Timu ya West Ham United inatarajiwa kuachana na kocha wake, Nuno Espirito Santo, kufuatia kushuka daraja kutoka Ligi Kuu England hadi Championship.

Kocha huyo raia wa Ureno mwenye umri wa miaka 52, kwa sasa yupo kwenye mazungumzo na bodi ya klabu hiyo baada ya safari ya miaka 14 ya West Ham kwenye ligi hiyo kuhitimishwa katika mchezo wa mwisho wa msimu jana, Jumapili, Mei 24, 2026.

Chini ya makubaliano ya mkataba wa miaka mitatu aliosaini mwezi Septemba, kocha huyo wa zamani wa Wolves na Tottenham Hotspur anaruhusiwa kuondoka klabuni hapo iwapo timu itashuka daraja. Vilevile, West Ham ina uwezo wa kusitisha mkataba ambao ungefikia thamani ya Pauni 8 milioni kwa mwaka zikiwemo bonasi za kubaki Ligi kuu bila kulipa fidia yoyote kutokana na kipengele hicho cha mkataba.

NU 01

Nuno alikabidhiwa mikoba baada ya mechi tano za msimu huu kuanza, akichukua nafasi ya Graham Potter. Kabla ya hapo alikuwa amefukuzwa kazi na Nottingham Forest baada ya mechi tatu za mwanzo. 

NU 02

Wakati Potter anafukuzwa, West Ham ilikuwa na pointi tatu tu, na imemaliza msimu ikiwa na alama 39, idadi kubwa zaidi ya alama kwa timu inayoshuka daraja tangu Birmingham City na Blackpool zilipofanya hivyo mwaka 2011.

Baada ya ushindi wa West Ham dhidi ya Leeds United jana Jumapili, Nuno alikataa kuzungumzia mustakabali wake, akieleza kuwa jambo hilo si kuhusu yeye, bali ni wakati mgumu kwa klabu, na kusisitiza kuwa West Ham inapaswa kurejea Ligi Kuu huku akitaka wapitie kwanza kipindi hiki cha huzuni kwa mashabiki.

Wakati Nuno akiondoka, kiungo wa zamani wa Hammers, Scott Parker, anatajwa kuwa miongoni mwa watakaowania nafasi hiyo baada ya kuondoka Burnley kabla ya msimu kufikia kikomo. 

Hata hivyo, West Ham inakabiliwa na kibarua kigumu cha kuuza wachezaji msimu huu wa kiangazi ili kupata zaidi ya pauni milioni 100 kutokana na mgogoro wa kifedha, huku nyota kama Jarrod Bowen, Mateus Fernandes, Tomas Soucek, na Crysencio Summerville wakitarajiwa kuondoka.