Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Botafogo yamfuta kazi kocha Paiva

BOTAFOGO Pict

MIAMI, MAREKANI: BOTAFOGO imemfuta kazi kocha Renato Paiva saa 48 baada ya timu hiyo kutupwa nje ya fainali za Kombe la Dunia la Klabu huko Marekani.

Miamba hiyo ya Brazil ilisukumwa nje ya michuano hiyo na Wabrazili wenzao, Palmeiras katika hatua ya 16 bora. Staa Paulinho alifunga bao pekee katika mechi hiyo dakika ya 100 baada ya kuongezwa dakika 30, kufuatia sare ya 0-0 baada ya dakika 90.

Na jambo hilo liliwafanya Botafogo kuchukua uamuzi wa kumwondoa kocha wao Paiva. Huo ni uamuzi wa mmiliki, ambaye alikuwa mmiliki mwenza wa Crystal Palace, John Textor kuthibitisha hilo kupitia mtandao wa kijamii usiku wa Jumapili.

Taarifa hiyo ilisomeka: “Botafogo inatangaza kwamba Renato Paiva hataendelea kuwa kocha wetu mkuu wa kikosi cha kwanza. Uamuzi huu tulikubaliana kiungwana. Klabu inamshukuru Paiva na benchi lake la ufundi kwa kipindi chote alichokuwa nasi.”

Botafogo ilitinga hatua ya 16 bora baada ya kumaliza katika nafasi ya pili kwenye Kundi B. Klabu hiyo iliwachapa mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Paris Saint-Germain na Seattle Sounders kwenye hatua ya makundi na hivyo kupenya kwenye kundi ambalo lilikuwa na Atletico Madrid pia.

Botafogo ilimaliza katika nafasi ya nane kwenye ligi ya Brazil, Serie A msimu uliopita na kukata tiketi ya kucheza hatua ya makundi kwenye CONMEBOL Sudamericana.