Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barcelona yatuma watu kumtazama Greenwood

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa taarifa kutoka tovuti ya TBR Football, klabu hiyo ya Catalonia imekuwa ikimfuatilia Greenwood kwa miezi kadhaa kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu ajiunge na Marseille akitokea Manchester United.

MASKAUTI wa Barcelona walikuwepo uwanjani mwishoni mwa wiki iliyopita kumtazama mshambuliaji wa Marseille, Mason Greenwood, 24.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka tovuti ya TBR Football, klabu hiyo ya Catalonia imekuwa ikimfuatilia Greenwood kwa miezi kadhaa kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu ajiunge na Marseille akitokea Manchester United.

Tangu kuanza kwa msimu huu alifunga mabao saba katika mechi 10 za michuano yote, pia ametoa asisti nne.

Mkataba wa fundi huyu unatarajiwa kumalizika mwaka 2029 na  Marseille inaripotiwa kuhitaji zaidi ya Euro 50 milioni ili kumuuza.

Licha ya nia ya kumhitaji, Barca inaoneana kuwa na uwezekano mdogo wa kulipa kiasi cha pesa kinachohitajika, hivyo huenda ikaomba ipunguziwe au ikamsajili kwa mkopo wa nusu msimu.


Samuel Omorodion

CHELSEA imeonyesha ipo tayari kutoa Euro 100 milioni ili kumsajili mshambuliaji wa FC Porto, Samuel Omorodion,mwenye umri  wa miaka 21, dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Omorodion, ambaye ana asili ya Nigeria lakini anachezea timu ya taifa ya Hispania ya vijana, msimu uliopita alicheza mechi 12 za michuano yote na kufunga mabao 10. Mkataba wake unamalizika mwaka 2029. Chelsea wanamwona kama mrithi sahihi wa Nicolas Jackson.


Lionel Messi

MSHAMBULIAJI wa Inter Miami na timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi, mwenye umri wa miaka 38, anatarajiwa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia katika klabu hiyo. Messi, ambaye alimaliza msimu wa 2025 kama mfungaji bora wa Ligi Kuu Marekani akiwa na mabao 29, ameendelea kuwa staa muhimu wa timu hiyo inayomilikiwa na nyota wa zamani wa Manchester United, David Beckham. Mkataba huo mpya unatarajiwa kuwa wa miaka miwili.


Djylian N’Guessan

ARSENAL na Tottenham Hotspur, zipo katika vita kali ya kuiwania saini ya mshambuliaji wa Saint-Etienne, Djylian N’Guessan,17, dirisha lijalo la majira ya baridi. N’Guessan amekuwa akitazamwa na maskauti wa timu nyingi Ulaya katika mechi mbalimbali ambazo pia zina mpango wa kutaka kumsajili. Klabu hiyo ni pamoja na Borussia Dortmund na AC Milan. Sporting inataka Euro 45 milioni ili kumwachia staa huyo.


Antoine Semenyo

BOURNEMOUTH imeweka wazi ipo tayari kupokea ofa  kwa  ajili ya kumuuza mshambuliaji wao wa kimataifa wa Ghana, Antoine Semenyo, mwenye umri wa miaka 25, katika dirisha lijalo la uhamisho. Ripoti zinaeleza klabu kadhaa kutoka Serie A na Bundesliga zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili staa huyu kutokana na kiwango bora ambacho amekionyesha akiwa na Bournemouth.

Mabosi wa Bournemouth wapo tayari kumuuza lakini kwa zaidi ya Euro 60 milioni. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2030.


Joel Ordonez

NEWCASTLE United na Aston Villa zinaonekana kuwa na nafasi kubwa zaiid ya  kumsajili beki wa kimataifa wa Ecuador, Joel Ordonez anayeichezea Club Brugge ya Ubelgiji. Kwa mujibu wa tovuti ya Caught Offside, klabu hizo mbili zinatamani sana kumsajili fundi huyu kwa sababu imevutiwa sana na uwezo wake wa kucheza kama beki wa kulia na beki wa kati.

Staa huyu  mwenye umri wa miaka 21, ana takwimu nzuri yakuwa beki aliyepiga pasi nyingi sahihi katika Ligi Kuu Ubelgiji.


Casemiro

MABOSI wa Manchester United, wanataka kumpa kiungo wao mkongwe kutoka Brazil, Casemiro, mkataba mpya wakati ule wa sasa ukitarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu. Casemiro,33, anatarajiwa kupewa mkataba huo mpya  ambao utakuwa na mabadiliko katika mshahara kutoka Pauni 350,000 kwa wiki anaoupata sasa hadi Pauni 200,000 kwa wiki.

Kiungo huyu alijiunga  na Man United akitokea Real Madrid mwaka 2022 kwa dau la Euro 70 milioni.


Bruno Fernandes

KAPTENI wa Manchester United, Bruno Fernandes, 31, anaripotiwa kufikiria kuondoka mwisho wa msimu huu ikiwa timu itaendelea kufanya vibaya. Kwa mujibu wa tovuti ya Fichajes, kiungo huyo amekuwa akihisi kukata tamaa kutokana na mwenendo wa timu hiyo kwani anahitaji kupata mataji. Timu kibao zinataka kumsajili staa huyu lakini mara zote ambazo zimewasilisha ofa Bruno mwenyewe alikataa.