Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barca, Real Madrid mguu sawa kwa Marc Guehi

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Guehi aliyewahi kuichezea Chelsea kabla ya kujiunga na Palace amekuwa mmoja wa mabeki waliodumu katika kiwango bora kwenye Ligi Kuu England na mbali ya vigogo hao wa Hispania, huduma yake pia inahitajika na Bayern Munich.

BARCELONA na Real Madrid zinafuatilia kwa karibu suala la beki wa kati wa Crystal Palace na timu ya taifa ya England, Marc Guehi, 25, ambaye ameonyesha nia ya kutosaini mkataba mpya wakati ule wa sasa ukitarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu.

Guehi aliyewahi kuichezea Chelsea kabla ya kujiunga na Palace amekuwa mmoja wa mabeki waliodumu katika kiwango bora kwenye Ligi Kuu England na mbali ya vigogo hao wa Hispania, huduma yake pia inahitajika na Bayern Munich.

Awali, beki huyo ambaye ni nahodha pia wa Palace alikuwa akihitajika na Liverpool iliyokaribia kumnunua kwa Pauni 30 milioni katika dirisha lililopita. Hata hivyo, Liverpool imeachana na mpango huo kwa sasa na inaangalia uwezekano wa kusajili mwingine.

Barca na Madrid zimevutiwa sana na kiwango cha Guehi pia wanaona itakuwa rahisi kumsajili kutokana na muda wa mkataba wake unaomalizika mwisho wa msimu huu.


Morten Hjulmand

KIUNGO wa kati wa Sporting Lisbon, Morten Hjulmand 26, anatajwa kuwa katika rada za Manchester United inayotaka kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya baridi ili kuboresha eneo la kiungo. Man United ina matumaini ya kumnasa raia huyo wa Denmark kwa ada ya takriban Pauni 50  milioni, ingawa bei inaweza kuzidi ikiwa vigogo wengine pia watataka kuingia katika vita ili kumpata. Kocha wa Man United, Ruben Amorim anadaiwa kuwa shabiki mkubwa wa staa huyo.


Samu Omorodion

MMSHAMBULIAJI wa FC Porto, Samu Omorodion mwenye  umri wa miaka 21 amewekwa kwenye orodha ya wachezaji wanaowaniwa na Tottenham Hotspur katika dirisha lijalo la usajili. Omorodion amekuwa akionyesha kiwango bora Porto tangu msimu uliopita. Spurs inataka kusuka upya safu ya ushambuliaji na imaamini fundi huyo ataziba pengo la Harry Kane ambaye tangu aondoke limekuwa likiyumba. Mkataba wa Omorodion unamalizika 2029.


Jurrien Timber

ARSENAL inaendelea na juhudi za kumshawishi beki wa kimataifa wa Uholanzi, Jurrien Timber, 24, kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia katika kikosi. Benchi la ufundi la Arsenal linajitahidi kuhakikisha kuwa Timber anabaki kwa sababu ni sehemu ya mipango yao. Inaelezwa Washika Mitutu wanataka kumsainisha mkataba wa muda mrefu ambao utamwezesha kupata kiasi kikubwa cha mshahara.


Guela Doue

BEKI wa Strasbourg, Guela Doue, 23, anafuatiliwa kwa karibu na timu kibao za Ligi Kuu England ambazo ni Chelsea, Aston Villa, Brighton na Brentford. Hata hivyo, Chelsea inaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kumpata kwa sababu wamiliki wa timu hiyo ndio walewale wanaomiliki Strasbourg. Ripoti zinaeleza Strasbourg ipo tayari kumwachia fundi huyo kwenda kusaka malisho mapya katika klabu zingine.


Takefuso Kubo

ASTON Villa inamfuatilia kwa karibu winga wa Rea Sociedad na Japan, Takefusa Kubo, 24, ambaye ameshawasilisha maombi ya kutaka kuondoka katika dirisha lijalo. Kubo anadaiwa kuwaambia mabosi wa Sociedad anataka changamoto mpya sehemu nyingine. Aston Villa inaandaa ofa ya zaidi ya Pauni 30 milioni ili kumpata fundi huyo. Hata hivyo, Sociedad inadaiwa kuhitaji zaidi ya Pauni 40 milioni.


Issouf Sissokho

LLEEDS United imeonyesha kuvutiwa na kiungo wa kati wa Maccabi Tel Aviv, Issouf Sissokho, 23, ambaye ni raia wa  Mali. Mabosi wa Leeds wanataka kumsajili staa huyu katika dirisha  lijalo la majira ya baridi. Sissokho amekuwa mchezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Maccabi na Leeds imekuwa ikimfuatikia kwa muda mrefu. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2027.


Vitalii Mykolenko

BEKI wa kushoto wa Everton na timu ya taifa ya Ukraine, Vitalii Mykolenko, 26, yupo katika rada za timu mbalimbali Italia na Hispania zinazotaka kumsajili katika dirisha lijalo la majira ya baridi. Inaelezwa miongoni mwa zile zinazotaka huduma yake ni pamoja na Napoli na Barcelona. Mabosi wa Everton wamekuwa wakipambana ili kumsainisha mkataba mpya ila wameshindwa.