Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bayern kuvuna Sh14 bil kucheza Kenya

BAYERN Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na vyombo mbalimbali vya habari, miamba hiyo ya soka kutoka Ujerumani inatarajiwa kulipwa kiasi hicho kwa kushiriki mchezo huo, ingawa Bayern na Ajax bado hazijathibitisha rasmi taarifa hizo.

MUNICH, UJERUMANI: MABINGWA WA Ujerumani, Bayern Munich inatarajiwa kuingiza Euro5 milioni(takribani Sh14 bilioni) kupitia mechi yake ya kirafiki dhidi ya Ajax Amsterdam utakaopigwa Januari 5, 2027, jijini Nairobi, Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na vyombo mbalimbali vya habari, miamba hiyo ya soka kutoka Ujerumani inatarajiwa kulipwa kiasi hicho kwa kushiriki mchezo huo, ingawa Bayern na Ajax bado hazijathibitisha rasmi taarifa hizo.

Mchezo huo utafanyika katika Uwanja wa Kimataifa wa Raila Odinga wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000. Unatarajiwa pia kuwa sehemu ya hafla ya uzinduzi wa uwanja huo mpya uliojengwa katika maandalizi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, ambazo Kenya itaandaa kwa pamoja na Tanzania na Uganda.


BAYE 01

KASPER AONGOZA MAANDALIZI

Ziara hiyo ni sehemu ya mkakati wa Bayern Munich wa kupanua ushawishi wake katika masoko ya kimataifa. Mjumbe wa bodi ya utendaji ya klabu hiyo, Rouven Kasper, ambaye anasimamia masuala ya masoko na mauzo, anaripotiwa kuwa mstari wa mbele katika kuratibu maandalizi ya mchezo huo.

Lengo ni kuimarisha uwepo wa Bayern katika soko la Afrika na kukuza uhusiano wake na mashabiki wengi wa klabu hiyo waliopo barani humo.

Kocha wa Bayern, Vincent Kompany, pia anaripotiwa kuridhia safari hiyo, ambayo itaiwezesha klabu hiyo kuunganisha malengo yake ya kibiashara na kujitangaza kimataifa.


BAYE 02

KENYA KUPATA FURSA YA KIMATAIFA

Mbali na kukutanisha klabu mbili kubwa za Ulaya, mchezo huo unatarajiwa kuwa fursa muhimu kwa Kenya kuitangaza miundombinu yake ya michezo kimataifa.

Uwepo wa Bayern na Ajax jijini Nairobi utaipa hadhi mpya Uwanja wa Kimataifa wa Raila Odinga na kuongeza mwonekano wa Kenya katika ramani ya soka duniani, miezi michache kabla ya kuanza kwa AFCON 2027.

Kwa Bayern, malipo yanayoripotiwa ya Euro5 milioni kwa mchezo mmoja yanaonyesha umuhimu unaoongezeka wa soko la Afrika katika mikakati ya kibiashara ya klabu kubwa za Ulaya.

BAYE 03

Hivyo, Januari 5, 2027, Nairobi inatarajiwa kuwa kitovu cha mvuto wa soka, huku miamba hiyo miwili ya Ulaya ikikutana katika ardhi ya Afrika.