Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bao la Henry

Mwandishi Wetu BAO lililofungwa na kiungo wa kimataifa wa Tanzania anayechezea timu ya Kongsvinger, Henry Joseph huenda likapata tuzo ya bao bora la mzunguko wa 13 wa Ligi Kuu ya Norway kutokana na kuongoza kwa kura. Katika mzunguko huo jumla ya mabao 22 yalifungwa na mabao matano kupita kwenye vigezo vilivyowekwa na sasa yanasubiri kura kutoka kwa mashabiki ili kupata bao bora zaidi. Joseph alifunga bao hilo kwa shuti la umbali wa mita 30 lililokwenda moja kwa moja wavuni katika mchezo wao dhidi ya Baerum. Hilo ni bao la kwanza kwa Henry kufunga katika Ligi Kuu ya Norway tangu alipojiunga na Kongsvinger miaka minne iliyopita na sasa anategemea kuweka rekodi ya kucheza mechi 60 za ligi akiwa na timu hiyo. Katika orodha ya wachezaji watano wanaowania tuzo hiyo Joseph Shindika wa Kongsvinger anaongoza kwa kupata asilimia 57.3% za kura akifutiwa na Daniel Fredheim wa Holm (21.3%), John Kamara wa Stromsgodset (13.6%), Julius Norbye Tromso wa Rosenborg (5%) na John Chibuike, Rosenborg (2.8%), mwisho wa kupigwa kura hizo ni Jumatano. Nahodha huyo wa zamani wa Tanzania, Henry alisema amefurahi kuona goli lake limeingia kwenye orodha ya mabao yanayowania tuzo hiyo. "Sasa nimefurahi baada ya kucheza kwa muda mrefu hatimaye Nimefunga bao hapa," alisema Henry ambaye kwa sasa ni baba wa mtoto wa kiume aliyemwita kwa jina la Ethan.