Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Babake Yamal asema Dembele hakustahili Ballon d’Or

YAMAL Pict

Muktasari:

  • Jana ulikuwa usiku wa sherehe kwa Dembele ambaye alishinda Ballon d’Or kwa mara ya kwanza baada ya msimu wa kushangaza akiwa na Paris Saint-Germain, ambapo Yamal (18), alimaliza katika nafasi ya pili.

PARIS, UFARANSA: BABA mzazi wa winga wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Lamine Yamal amesema mchezaji sahihi hakuwa ameshinda tuzo ya Ballon d’Or baada ya Ousmane Dembele kushinda, akisisiza kwamba "kitu kigeni kimejitokeza" mwaka huu.

Jana ulikuwa usiku wa sherehe kwa Dembele ambaye alishinda Ballon d’Or kwa mara ya kwanza baada ya msimu wa kushangaza akiwa na Paris Saint-Germain, ambapo Yamal (18), alimaliza katika nafasi ya pili.

Yamal alipata zawadi ya faraja ya Tuzo ya Kopa kwa mwaka wa pili mfululizo ambayo hata hivyo, baba yake, Mounir Nasraoui hakuifurahia sana akiahidi kuwa mwanawe ni lazima ashinde Ballon d’Or mwakani. Tuzo hiyo huchukuliwa na wachezaji bora chini ya umri wa miaka 21.

Nasraoui alishutumu mfumo wa upigaji kura wa Ballon d’Or akidai "unaumiza", lakini kwa sababu imetokea hakuna jinsi isipokuwa haridhishwi na kilichotokea, kwani mwanawe alifanya mambo mengi zaidi ya Dembele msimu uliopita.

Itakumbukwa kwamba mchezaji huyo aliisaidia Hispania kubeba ubingwa Euro 2024, ubingwa wa Laliga akiwa na Barcelona huku akitembea na rekodi tamu katika maeneo mbalimbali uwanjani ikiwamo ufungaji wa mabao 18, asisti 25 na pia umiliki wa mpira.

“Yeye ndiye bora zaidi. Sitaki kusema vibaya, bali nachosema inaumiza kibinadamu. Lamine Yamal ndiye mchezaji bora zaidi duniani kwa mbali. Sio kwa sababu yeye ni mwanangu tu, bali kwa sababu ndiye mchezaji bora zaidi duniani. Lamine ni Lamine… Kitu kigeni kimejitokeza hapa. Mwaka ujao ni wetu. Ballon d’Or itakuwa kwa Mhispaniola,” alisema mzazi huyo huku nyuma ya Yamal aliyeshika nafasi ya tatu akiwa ni kiungo wa PSG, Vitinha.

Hata hivyo, Yamal aliwashukuru waandaji wa tuzo akisema: “Kwanza kabisa asante kwa France Football kwa tuzo hii. Ni heshima kuwa hapa tena. Ningependa pia kuishukuru klabu yangu Barcelona na timu ya taifa kwa kuwa bila wao nisingekuwa hapa.”

Kocha wa Barcelona, Hansi Flick, alionyesha heshima kwa Yamal akisema tuzo aliyoipata ni ushahidi wa mafanikio yake.

“Sijui kama atashinda Ballon d’Or. Lakini, nina uhakika kwamba siku moja tutaona Lamine akishinda. Ni heshima tu kutajwa.”

Dembele, mwenye miaka 10 zaidi ya Yamal alishinda kwa tofauti kubwa ya kura kulingana na mhariri mkuu wa France Football, Vincent Garcia.

“Ousmane alishinda kwa sapoti kubwa kutoka kwa majaji wetu wa Ballon d’Or. Hakukuwa na usambazaji mkubwa wa kura. Vitinha na Achraf Hakimi walipata kura chache tu. Ousmane Dembele alishinda kwa kiwango cha kimataifa, Ulaya, Amerika Kusini na Amerika Kaskazini… Hii ni Ballon d’Or ya wazi na isiyopingika.”