Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ATM YA WIKI: Heshima NBA imempa utajiri Jordan

ATM Pict

Muktasari:

  • Licha ya kutotajirika wakati anacheza kikapu, Michael amejikuta akifikia ubilionea mara baada ya kustaafu kutokana na biashara anazozifanya kwa sasa pamoja na mkataba wake na Nike ambao unamwezesha kupata pesa nyingi kwa kutumia tu jina lake katika viatu hivyo.

CHICAGO, MAREKANI: MOJA kati ya viatu maarufu duniani ni Air Jordan ambavyo vimebeba jina la mchezaji wa zamani wa kikapu wa Marekani Michael Jordan.

Licha ya kutotajirika wakati anacheza kikapu, Michael amejikuta akifikia ubilionea mara baada ya kustaafu kutokana na biashara anazozifanya kwa sasa pamoja na mkataba wake na Nike ambao unamwezesha kupata pesa nyingi kwa kutumia tu jina lake katika viatu hivyo.

Leo tumekusogezea hapa, utajiri wake kwa jumla na jinsi anavyopiga pesa.


AT 04

ANAPIGAJE PESA

Kijumla ana utajiri unaofikia Dola 3.5 bilioni unaotokana na biashara zake, pesa za mshahara alipokuwa anacheza pamoja na mikataba ya udhamini.

Michael ana mkataba wa udhamini na kampuni mbalimali ikiwa pamoja na Gatorade, Wheaties, McDonald’s, Coca-Cola, Chevrolet, Ball Park Franks, Rayovac, Hanes, MCI, Upper Deck, 2K Sports na Five Star Fragrances.

Staa huyu pia anamiliki duka kubwa la magari na migahawa saba ya uuzaji wa chakula.

AT 02

Mkataba mkubwa zaidi wa udhamini ambao unazidi kumpa jeuri hadi sasa ni ule wa Nike ambao ni maalumu kwa ajili ya kutumia jina lake katika brandi za viatu. Mkataba huo unamwezesha kupata Dola 60 milioni kila mwaka.

Pia umiliki wake wa hisa asilimia nyingi za timu ya NBA ya Charlotte Hornets unamwongezea utajiri na amewekeza takriban Dola 170 milioni, sasa hisa za timu hiyo zimepanda thamani na akiamua kuziuza huenda akapata hadi Dola 1 bilioni.


AT 03

MIJENGO

Kwa sasa nyuma anayoishi ni yakifahari iliyopo huko Jupiter, Florida. Nyumba hiyo ina vyumba 11 na ukubwa wa futi za mraba 26,000 ipo kwenye eneo la eka tatu.

Alinunua eneo hilo mwaka 2011 kwa Dola 4.8 milioni, kisha alitumia miaka miwili na dola milioni 7.6 kujenga nyumba ya ndoto yake.

Mnamo Machi 2013, Michael alilipa Dola 2.8 milioni kununua nyumba kubwa kwenye ziwa huko Charlotte, North Carolina.

Nyumba hiyo ina vyumba sita vya kulala na bafu nane. Ipo kwenye kiwanja cha takriban futi za mraba 50,000, pia ana nyumba nyingine maeneo ya Salt Lake City, Utah.

Huko Chicago, Michael bado anamiliki jumba kubwa la kifahari katika Highland Park.


AT 01

NDINGA

Ford F-150 Raptor - Dola 85,000

Ferrari 599 GTB Fiorano  - Dola 150,000

Mercedes-Benz SLR McLaren 722 Edition - Dola 500,000

Ferrari 512 TR (1992-1994) -Dola 150,000

Mercedes-Benz SL 55 AMG-Dola 35,000

Porsche 911-Dola 200,000

Chevrolet C4 Corvette -Dola 25,000

Chevrolet Corvette ZR1-Dola 35,000

Aston Martin DB9 Volante-Dola 70,000

Mercedes-Benz CL 65 -Dola 55,000

Aston Martin DB7 Volante-Dola 50,000

Cadillac XLR-Dola 30,000


AT 05

NDEGE

Michael anamiliki ndege yake binafsi aina ya Gulfstream G550 yenye thamani ya Dola 50 milioni ambayo huitumia kwenye mizunguko yake sehemu mbalimbali duniani.

Ndege hii ina alama maarufu ya ‘Jumpman’ ya Michael kwenye mkia, na nambari yake ya usajili ni N236MJ (ikionyesha nambari yake ya jezi na herufi za jina la staa huyu),  ilijengwa mwaka 2005 na ina injini ya Rolls-Royce BR 700 Series Turbo Fan.


MAISHA NA BATA

Staa huyu alimuoa Juanita Vanoy mnamo Septemba 1989. Walifanikiwa kupata  watoto watatu pamoja. Walipoachana mmwaka 2002 baada ya kudumu kwa miaka 13, Jordan alilazimika kumlipa mwanamke huyu fidia ya Dola 168 milioni na ikatajwa ni mojawapo ya talaka ghali zaidi katika historia. Makubaliano hayo yalijumuisha pesa taslimu, hisa, na thamani ya mali zao mbalimbali walizochuma wakiwa pamoja.

Kwa sasa yupo kwenye ndoa na mrembo Yvette Prieto aliyemuoa Aprili 2013 na amezaa naye watoto wawili. Mwaka 2019, Jordan alikua babu baada ya binti yake Jasmine kujifungua mtoto wa kiume.