Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal yapewa tahadhari kwa Osimhen

Muktasari:

  • The Gunners wameonesha nia ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Nigeria wakati wakiendelea kufanya mazungumzo na Galatasaray, ambayo yenyewe pia inawafuatilia baadhi ya nyota wa Arsenal.

LONDON, ENGLAND

Galatasaray tayari imekataa ofa yenye thamani ya pauni  111 milioni kutoka kwa klabu ya Saudi Arabia, Al-Hilal, kwa ajili ya mshambuliaji Victor Osimhen jambo linaloonesha kuwa ni kama onyo kwa Arsenal inayomtaka staa huyo.

The Gunners wameonesha nia ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Nigeria wakati wakiendelea kufanya mazungumzo na Galatasaray, ambayo yenyewe pia inawafuatilia baadhi ya nyota wa Arsenal.

Galatasaray imedhamiria kumbakiza mshambuliaji wake huyo nyota na haitaki kumuuza.

Uamuzi wao wa kukataa zaidi ya pauni 100 milioni katika majira haya ya kiangazi unaashiria kwamba Arsenal italazimika kutoa zaidi ya kiasi hicho ili kumnasa Osimhen, jambo ambalo lingekuwa matumizi makubwa zaidi ya fedha katika historia ya klabu hiyo.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Napoli amekuwa akihusishwa na kuhamia Ligi Kuu England mara kadhaa katika maisha yake ya soka, huku Chelsea ikiwa miongoni mwa klabu zilizowahi kumfuatilia kwa karibu.

Hata hivyo, wakati wake nchini Italia ulipofika mwisho, alihamia Galatasaray, ambako amesaidia klabu hiyo kuwa mabingwa.

Osimhen mwenye umri wa miaka 27 alifunga mabao 22 katika mashindano yote msimu uliopita.

Arsenal bado inaendelea na mazungumzo na klabu hiyo ya Uturuki huku ikijaribu kumuondoa Gabriel Martinelli na, ikiwezekana, Ethan Nwaneri, kwa mujibu wa The Sun.

Galatasaray imeashiria kuwa iko tayari kulipa karibu pauni 38 milioni kwa ajili ya Martinelli, ambaye wakati mmoja alikuwa miongoni mwa wachezaji waliopendwa zaidi Arsenal, lakini sasa ameshuka.

Hata hivyo, kiasi hicho bado kingekuwa faida kubwa kwa Arsenal, ambayo ilimsajili Mbrazil huyo mwaka 2019.  Nwaneri ni mchezaji mwingine ambaye amepoteza nafasi kutokana na sera kali ya Arsenal katika usajili wa wachezaji katika miaka ya hivi karibuni.

Kijana huyo alilazimika kwenda Marseille kwa mkopo msimu uliopita na baada ya kurejea Kaskazini mwa London, inaaminika kwamba anapendelea kuhamia Ujerumani iwapo ataondoka Arsenal.

Borussia Dortmund na RB Leipzig zote zinamtaka.

Mikel Arteta yuko kwenye soko la usajili akitafuta mshambuliaji mkubwa katika dirisha hili la kiangazi, baada ya kukosa nafasi ya kuwasajili wachezaji kama Morgan Rogers na Vinicius Junior.

Wachezaji hao wote wangekuwa usajili mkubwa, huku Rogers hatimaye akihamia Chelsea kwa ada iliyoweka rekodi ya mchezaji wa Uingereza.

Inaripotiwa kwamba Arsenal ilikataa kufikia bei iliyowekwa na Chelsea, baada ya ada ya Rogers kwenda zaidi ya thamani ambayo klabu hiyo ilikuwa imeweka.

Osimhen, ambaye anakaribia kufikia kilele cha uwezo wake, ni aina tofauti ya mshambuliaji na mastraika wanaohakikisha mabao ni miongoni mwa mali ghali zaidi katika soko la usajili.

Arsenal ilitumia pauni  64 milioni kumsajili Viktor Gyokeres msimu uliopita, lakini Msweden huyo hakuonekana kushawishi kikamilifu katika msimu wake wa kwanza kwenye Uwanja wa Emirates.

Gyokeres aliachwa nje ya kikosi kilichocheza fainali ya Ligi ya Mabingwa, na Arteta sasa anataka kuongeza nguvu zaidi katika safu yake ya ushambuliaji.