Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal kusikilizia ofa za Trossard, Gabriel Jesus

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Mabosi wa Arsenal, wanataka kumuuza Jesus kwa sababu ya hali yake ya majeraha ya mara kwa mara ambayo amekuwa akiyapata na kwa sasa bado anaendelea kuuguza majeraha ya goti ambayo aliyoyapata mwanzoni mwa mwaka huu.

ARSENAL ipo tayari kupokea ofa za kuwauza mastaa wake akiwamo mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil, Gabriel Jesus, 28 (pichani) na winga wa Ubelgiji, Leandro Trossard, 30, katika dirisha lijalo la majira ya baridi.

Mabosi wa Arsenal, wanataka kumuuza Jesus kwa sababu ya hali yake ya majeraha ya mara kwa mara ambayo amekuwa akiyapata na kwa sasa bado anaendelea kuuguza majeraha ya goti ambayo aliyoyapata mwanzoni mwa mwaka huu.

Hata hivyo, atakaporejea nafasi yake ya kucheza  katika kikosi cha kwanza mbele ya Viktor Gyokeres na Kai Havertz haionekani kuwa kubwa.

Taarifa zinadai kwamba kwa upande wa Trossard ni yeye mwenyewe ndiye ameonyesha nia ya kutaka kuondoka kwa sababu hapati nafasi ya kutosha.

Mkataba wa Jesus unatarajiwa kumalizika ifikapo 2027 wakati ule wa Trossard ukitarajiwa kumalizika 2027.


Kobbie Mainoo

KIUNGO wa Manchester United, Kobbie Mainoo mwenye umri wa miaka 20 huenda akaomba tena kujiunga kwa mkopo na Napoli Januari, mwakani, iwapo hatapatiwa nafasi kubwa ya kucheza kwenye kikosi cha Mashetani Wekundu. Mainoo alikuwa akitaka kuondoka katika dirisha lililopita la majira ya kiangazi, lakini ilishindikana baada ya Man United kugoma kumwachia.


Micky van de Ven

REAL Madrid ina nia ya kumsajili beki wa kati wa Tottenham Hotspur, Micky van de Ven mwenye umri wa miaka 24 kuelekea dirisha lijalo la majira ya baridi. Mabosi wa Spurs wapo tayari kumuuza beki huyo wa kimataifa wa Uholanzi kwa dau la takriban Pauni 70 milioni. Van de Ven alijiunga na Spurs akitokea Wolfsburg 2023 kwa takriban Euro 40 milioni na amekuwa miongoni mwa mabeki tegemeo wa timu hiyo.


Jean-Philippe Mateta

MSHAMBULIAJI wa Crystal Palace na Ufaransa, Jean-Philippe Mateta, 28, hana mpango wa kujiunga na Leeds United licha kuwasilisha ofa ya kutaka kumsajili na badala yake anataka  kuhamia Aston Villa. Mateta amekuwa na kiwango bora tangu msimu uliopita kiasi cha kuvutia vigogo mbalimbali waliohitaji kumsajili katika dirisha lililopita lakini ilishindikana.


Lukasz Fabianski

WEST Ham United inafanya mazungumzo ya kumsajili tena kipa wa Poland, Lukasz Fabianski, 40, ikiwa ni miezi miwili baada ya kuondoka. Fabianski aliyewahi pia kucheza Arsenal na Swansea kwa sasa yupo huru na anaruhusiwa kujiunga na timu yoyote Ulaya. West Ham United inataka kumrudisha kama kipa wa akiba nyuma ya Alphonse Areola.


Zeno Debast

MMANCHESTER United inataka kumsajili beki wa kati wa Sporting Lisbon na timu ya taifa ya Ubelgiji, Zeno Debast, 21, katika dirisha lijalo la majira ya baridi mara tu litakapofunguliwa, lakini Arsenal na Aston Villa pia zinafuatilia saini yake kwa karibu. Debast ni mmoja wa mabeki chipukizi bora  Ulaya kwa sasa aliyesajiliwa Sporting Lisbon akitokea Anderlecht. Sporting inahitaji takriban Pauni 40 milioni ili kumuuza mchezaji huyo.


Yves Bissouma

KIUNGO wa Tottenham Hotspur na timu ya taifa ya Mali, Yves Bissouma, 29, anatarajiwa kuondoka katika dirisha lijalo la majira ya baridi baada ya kupoteza nafasi chini ya kocha mpya Thomas Frank. Bissouma alijiunga Spurs kutoka Brighton 2022, lakini hivi karibuni amekuwa akikumbana na majeraha ya mara kwa mara. Timu kadhaa za Italia na Saudia zinahitaji huduma yake.


Adam Wharton

LIVERPOOL na Newcastle United ni miongoni mwa timu mpya zilizoingia kwenye kinyang’anyiro cha kutaka kumsajili kiungo wa Crystal Palace na timu ya taifa ya England, Adam Wharton, 21, katika dirisha lijalo la majira ya baridi. Awali, Chelsea na Manchester United ndizo zilizoripotiwa kutaka kumsajili staa huyo katika dirisha lililopita lakini zilishindwa kufikia mwafaka na Palace.