Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim sasa ashtuka! Afichua siri AC Milan

AMORIM Pict

Muktasari:

  • Amorim, 41, ameanza vyema safari yake Serie A, akiongoza AC Milan kutopoteza katika michezo yake mitano ya kwanza baada ya kuichapa Lecce mabao 3-0 mwishoni mwa wiki.

MILAN, ITALIA: KOCHA wa zamani wa Manchester United, Ruben Amorim, amekiri kuwa alifanya makosa wakati wa kuinoa klabu hiyo ya England, huku akisema amejifunza kutokana na yaliyompata na sasa anatumia uzoefu huo kuijenga AC Milan.

Amorim, 41, ameanza vyema safari yake Serie A, akiongoza AC Milan kutopoteza katika michezo yake mitano ya kwanza baada ya kuichapa Lecce mabao 3-0 mwishoni mwa wiki.

Ushindi huo umeifanya Milan kufikisha pointi 11 katika mechi tano na kushika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi.

Baada ya mchezo huo, Amorim amesema kuwapa wachezaji uhuru zaidi wa kucheza kulikuwa miongoni mwa sababu zilizowasaidia kupata ushindi huo.

Kocha huyo Mreno pia alikiri kuwa uamuzi huo unatokana na somo alilolipata wakati akiwa Manchester United.

“Tumeboresha mambo mengi. Uhuru wa wachezaji, namna walivyokuwa wakisogea na hasa mbio za kwenda nyuma ya safu ya ulinzi. Hatukuwa timu inayomiliki mpira tu, bali pia tulikuwa timu yenye uwezo wa kuwa hatari,” amesema Amorim.

Ameongeza: “Tulikuwa na nafasi za kukimbilia na hilo ni jambo zuri. Tulidhibiti mchezo na tulielewa kuwa wapinzani walikuwa wakingojea tufanye makosa, lakini tulilinda vizuri na tulistahili kushinda.”


AMOR 01

‘SIWEZI KURUDIA MAKOSA

Amorim alipoelezwa kuhusu kilichosababisha mabadiliko hayo, amesema amekuwa akitazama kwa karibu michezo pamoja na kuelewa uwezo na tabia za wachezaji wake.

“Ni uchunguzi wa michezo na sifa za wachezaji. Bila shaka ninawasikiliza wachezaji, lakini kocha wa timu kubwa lazima awasikilize wachezaji, awaone na kuwaelewa,” amesema.

Hata hivyo, amesisitiza kuwa kocha anapaswa kusimamia utambulisho wa timu bila kupuuza uwezo wa wachezaji alionao.

“Kila mchezaji anataka mchezo uelekee kwenye sifa zake. Kama unataka kuwa na utambulisho wa timu, hilo linaweza kuwa gumu,” amesema.

“Hatua zote ni maamuzi yangu. Nilichokiona kwenye michezo ya mwisho ndicho nilichokiona Manchester United, na siwezi kufanya kosa lilelile.”

Amorim amesema wakati mwingine timu haina wachezaji wenye sifa zinazohitajika kutekeleza mfumo fulani, hivyo kocha anapaswa kubadilika kulingana na mazingira.

“Wakati mwingine hatuna sifa kamili za kucheza kwa namna hiyo. Kama hatuna, tunapaswa kubadilika. Nadhani leo ilifanya kazi, lakini kwenye mchezo mwingine tunaweza kurudi kwenye ujenzi wa mashambulizi kwa kutumia mabeki watatu,” amesema.

“Cha muhimu ni kuwa na njia tofauti za kucheza.”


AMOR 02

HISTORIA YA MAN UNITED

Amorim pia amefanikiwa kuingia kwenye historia ya AC Milan baada ya kuwa kocha wa kwanza tangu Nils Liedholm mwaka 1963, kukusanya pointi 11 katika michezo yake mitano ya kwanza ya Serie A.

Hata hivyo, Amorim hakutaka kutawaliwa na rekodi hiyo, akisisitiza kuwa bado ana kazi kubwa mbele yake.

“Ni takwimu nzuri, lakini huu ni wakati tofauti. Tuna mambo mengi ya kufanya, lakini tunaboresha na tunajifunza,” amesema.

Kwa mujibu wa Amorim, changamoto kubwa katika michezo iliyopita ilikuwa mfumo wa timu kuwa mgumu kutokana na wachezaji kubaki kwenye nafasi zao kwa kiwango kikubwa.

“Katika michezo iliyopita tulikuwa na changamoto kwa sababu muundo ulikuwa umefungwa sana kwenye nafasi. Lakini wachezaji walipopata uhuru kidogo zaidi, walicheza vizuri zaidi,” amesema.


AMOR 03

UNITED ILIVYOMALIZIKA

Amorim alichukua mikoba ya Manchester United akiwa na matarajio makubwa, lakini mwanzo wake kwenye Premier League ulikuwa mgumu.

Katika michezo yake mitano ya kwanza akiwa United msimu uliopita, alikusanya pointi saba pekee.

Baadaye aliondolewa kwenye nafasi hiyo mwezi Januari, akimaliza kipindi chake cha takribani miezi 14 akiwa Old Trafford.

Sasa akiwa AC Milan, Amorim anaonekana kutumia uzoefu huo kurekebisha namna anavyosimamia timu, huku akisisitiza umuhimu wa kuwa na uwezo wa kubadilisha mfumo kulingana na wachezaji na wapinzani.