Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim atangaza msimamo ishu ya Kobbie Mainoo, Joshua Zirkzee

AMORIM Pict

Muktasari:

  • Kocha huyo kutoka Ureno amekiri kuwa wachezaji hao wawili wameonyesha kutoridhishwa na muda mdogo wa kucheza, lakini ameweka wazi kuwa bado ni wachezaji wa Man United na hawataruhusiwa kuondoka katikati ya msimu, kwani anatafuta namna ya kuwatumia ipasavyo.

Kocha Mkuu wa Manchester United, Ruben Amorim amezima uvumi unaodai kuwa wachezaji  Kobbie Mainoo na Joshua Zirkzee wanaweza kuondoka kwenye klabu hiyo ya Old Trafford, Januari 2026. 

Kocha huyo kutoka Ureno amekiri kuwa wachezaji hao wawili wameonyesha kutoridhishwa na muda mdogo wa kucheza, lakini ameweka wazi kuwa bado ni wachezaji wa Man United na hawataruhusiwa kuondoka katikati ya msimu, kwani anatafuta namna ya kuwatumia ipasavyo.

Mainoo, ambaye aliomba kupelekwa kwa mkopo mwishoni mwa dirisha la usajili la majira ya kiangazi, alikataliwa kwa sababu klabu ilimuona kama sehemu muhimu ya mipango yao ya msimu huu. 

Hata hivyo, kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20 hajaanza hata mechi moja ya Ligi Kuu na amejikuta nyuma ya Casemiro na Bruno Fernandes katika nafasi za kiungo, chini ya kocha Amorim.

Kwa upande mwingine, Zirkzee naye amekuwa na mwanzo mgumu msimu huu, kwani hadi sasa Muholanzi huyo amecheza mechi tatu tu za Ligi Kuu kama mchezaji wa akiba, pamoja na mechi moja ya Kombe la Carabao dhidi ya Grimsby Town, mwezi Agosti. 

AMO 02

Kutokuhusishwa kwake mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza cha Amorim, kumeibua tetesi za Zirkzee kurejea kwenye Ligi ya Italia (Serie A) kwa mkopo, huku AS Roma ikikihusishwa na nia ya kumsajili Januari 2026.

Amorim, ameweka wazi msimamo wake kufuatia uvumi unaowahusu wawili hao, kwa kuamini Mainoo na Zirkzee bado watakuwa na nafasi muhimu msimu huu, kutokana na mechi nyingi za Ligi kuwakabili.

Kocha huyo, ambaye amekuwa akikosolewa kwa uchaguzi wake wa wachezaji na kushindwa kubadilisha kikosi mara kwa mara, ametoa kauli hiyo wakati muhimu, kwani Man United inaendelea kusaka mwendelezo wa matokeo mazuri baada ya kuanza msimu kwa kusuasua.

 “Hiyo ni hali ya kawaida, na najua pia kuwa katika klabu yetu, kila kitu kinakuwa kelele nyingi lazima kifanywe kuwa habari kubwa mitandaoni. Kama inavyozungumzwa, kuna fainali za Kombe la Dunia, kuna mawakala wanaowafuatilia wachezaji kila wakati. Hivyo naelewa hilo, lakini hawa ni wachezaji wetu, na tunawahitaji wote wawili ili kuwa na msimu mzuri.”

AMO 01

Katika hatua nyingine, kocha huyo ameepuka kujibu moja kwa moja kauli ya Marcus Rashford aliyedai kuwa Man United inafanya kazi katika mazingira yasiyo sahihi, badala yake, Amorim amesema: “Ninajikita kwenye mustakabali wa klabu, na hali ya sasa ya klabu. Hilo ndilo jambo muhimu zaidi. Hivyo, ninazingatia wachezaji wangu tu, wanachosema, wanachofanya hiyo ndiyo kipaumbele changu.”