Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim aanika mbinu atakayoitumia dhidi ya Liverpool

MAN UTD Pict

Muktasari:

  • Everton, Manchester City, na timu ya taifa ya England inayonolewa na Thomas Tuchel zimekuwa zikitumia mbinu ya kupiga mipira mirefu msimu huu, na imekuwa ikiwasaidia kupata matokeo mazuri.

Hatimaye Kocha wa Man United, Ruben Amorim amekiri kujipanga kutumia mfumo mpya wa mipira mirefu katika mechi za Ligi Kuu ya England, baada ya kuwaambia wachezaji wake wamekosa makali, hivyo wanapaswa kutumia mbinu mbadala.

Everton, Manchester City, na timu ya taifa ya England inayonolewa na Thomas Tuchel zimekuwa zikitumia mbinu ya kupiga mipira mirefu msimu huu, na imekuwa ikiwasaidia kupata matokeo mazuri.

Kocha Amorim amewataka wachezaji wa Man United watumie mbinu hiyo sambamba na mbinu nyingine alizowahi kuwafundisha, ili kufanikisha mpango wa kupata matokeo chanya kwenye mechi zinazowakabili msimu huu 2025/26.

AMO 01

Akizungumza kabla ya mechi ya leo dhidi ya Liverpool, Amorim amesema: “Tuna wachezaji wenye sifa ya kuwa na nguvu za kutosha, haswa wanaocheza safu ya ushambuliaji, ninaamini mbinu ya kutumia mipira mirefu itatusaidia sana, 
Ninaamini kila hatua tunayopiga itakuwa na mabadiliko makubwa, nimekutana na wachezaji wangu na kuwaambia hili, mara kadhaa tumeifanyia mazoezi mbinu hii, na huenda tukaitumia kwenye mechi ya leo dhidi ya Liverpool.”

Ameongeza: “Kila wakati mpira unapokwenda kwa kipa, timu nyingi hucheza mtu kwa mtu lakini wakati mwingine huna mtu wa kumpasia. Senne Lammens anacheza kwa miguu yote miwili. Hivyo ni vigumu kwa timu kumpa presha kipa kutoka upande mmoja tu. Lakini bado lazima awe tayari.”

MAN 01

Katika Ligi Kuu ya EPL msimu huu, mabao yaliyotokana na mipira mirefu yameongezeka, huku idadi ya mipira mirefu ya kurusha (long throws) ikiongezeka mara mbili kwa kila mechi, wakati timu zinapunguza pasi nyingi na badala yake kupeleka mpira mbele kwa haraka.
Asilimia 48.4 ya mipira ya kuanzisha (goal kicks) huishia nusu ya uwanja ya wapinzani.

Amorim alitumia mbinu hizi za moja kwa moja (direct tactics) katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Sunderland, ambapo Diogo Dalot alipiga mipira mirefu, na ile ya kurusha moja kwa moja ndani ya eneo la hatari.
Na mpira wa kichwa wa Benjamin Sesko kwenda kwa Bryan Mbeumo ulimfanya kipa wa Chelsea, Robert Sanchez, apewe kadi nyekundu kwenye ushindi wa mwezi uliopita.

Ushindi dhidi ya Sunderland ulikuwa wa pili wa United katika mechi tatu zilizopita, lakini Amorim bado hajashinda mechi mbili mfululizo za ligi, tangu alipojiunga na klabu hiyo karibu mwaka mmoja uliopita.