Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyezimishwa ulingoni amkataa Mayweather

ORTIZ Pict

Muktasari:

  • Badala yake, Ortiz amemtaja Andre Berto kuwa ndiye bondia aliyempa changamoto kubwa zaidi. Anasema pambano lake na Berto lilikuwa na ushindani wa hali ya juu na lilimlazimisha kutumia uwezo wake wote kushinda.

TEXAS, MAREKANI: BONDIA wa Marekani, Victor Ortiz amesema kuwa hamchukulii Floyd Mayweather Jr. kama mpinzani bora zaidi aliyewahi kukutana naye ulingoni.

Kauli hiyo imewashangaza wengi, hasa ukizingatia mafanikio makubwa ya Mayweather katika ndondi.

Badala yake, Ortiz amemtaja Andre Berto kuwa ndiye bondia aliyempa changamoto kubwa zaidi. Anasema pambano lake na Berto lilikuwa na ushindani wa hali ya juu na lilimlazimisha kutumia uwezo wake wote kushinda.

Katika pambano lao la mwaka 2011, ambalo lilitajwa kama “Pambano Bora la Mwaka,” mabondia hao walionyesha kiwango cha juu  katika msumbwi. Wote wawili waliangushana chini mara mbili na pambano hilo lilikuwa la kusisimua kuanzia mwanzo hadi mwisho. Hatimaye, Ortiz alishinda kwa uamuzi wa majaji wote na kuchukua taji la uzito wa welter la WBC.

ORT 01

Ortiz anasema pambano hilo lilionyesha kila kitu ambacho bondia mkubwa anapaswa kuwa nacho. Kwa maoni yake, Berto alikuwa na nguvu, ustadi, moyo wa kupigana na uwezo wa kurejea hata baada ya kuangushwa. Ndiyo sababu anamwona kama mpinzani bora zaidi aliyewahi kukutana naye.

Baada ya ushindi huo, Ortiz alipata nafasi ya kupigana na Mayweather miezi michache baadaye. Hata hivyo, pambano hilo liliishia kwa njia yenye utata mkubwa uliovuta hisia za mashabiki wengi wa ndondi duniani.

Katika raundi ya nne ya pambano hilo, Ortiz alimgonga Mayweather kwa kichwa kwa makusudi. Kitendo hicho kilimfanya mwamuzi Joe Cortez kuingilia kati na kumpunguzia Ortiz pointi. Baada ya hapo, Ortiz alijaribu kuomba msamaha na hata kumkumbatia mpinzani wake.

Lakini wakati huo huo, Mayweather alitumia nafasi hiyo kwa haraka na kumpiga Ortiz ngumi kali ya kushoto ikifuatiwa na ya kulia. Ngumi hizo zilimwangusha Ortiz na kumpoteza fahamu na hivyo pambano kumalizika kwa ushindi wa Mayweather.

Tukio hilo liliacha mjadala mkubwa, kwani baadhi ya watu waliona kuwa lilikuwa halina uhalali, huku wengine wakiamini kuwa Mayweather alifuata sheria za mchezo kwa kutumia umakini wake.

ORT 02

Pamoja na hayo yote, Ortiz bado anaamini kuwa Mayweather si mpinzani bora zaidi aliyewahi kukutana naye. Ameeleza kuwa mtindo wa Mayweather haukuwa na changamoto kubwa kwake kama ule wa Berto, akidai kuwa Mayweather anategemea zaidi kujilinda na kushambulia kwa kujibu.

Hata hivyo, ukweli unabaki kuwa Mayweather ni mmoja wa mabondia bora zaidi katika historia ya ndondi.

Alihitimisha taaluma yake akiwa na rekodi ya ushindi wa mapambano 50 bila kupoteza na aliwashinda wapinzani wengi wakubwa, wakiwemo Berto mwenyewe katika moja ya mapambano yake ya mwisho.

Kwa upande mwingine, Berto aliendelea kuonyesha uwezo wake kwa kumshinda Ortiz katika pambano la marudiano kwa njia ya KO. Ushindi huo uliashiria kuporomoka kwa kiwango cha Ortiz na mwisho wa kipindi chake cha ubora katika ndondi.