Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fury, Usyk waletewa ‘Bwa mdogo’

NGUMI Pict

Muktasari:

  • Itauma mwenye miaka 21, amepanda kwa kasi kwenye uzito wa juu, rekodi yake sio ya kitoto, katika mapambano 14, hajapoteza hata moja huku 12 kati ya hayo yakimalizika kwa kumuangusha mpinzani wake ‘KO’, inaonyesha kuwa ni balaa lingine katika ngumi za uzito wa juu.

LONDON, ENGLAND: KAMA kawaida yao Waingereza wameanza kupigia kelele jambo lao, si unawajua walivyo wakiwa na la kuongea, sasa mdomoni mwao yupo Moses Itauma ambaye ni kati ya mabondia hatari ambao wanachipukia kwa kasi na tayari ameanza kutajwa kuwa huenda akazichapa na mmoja kati ya Tyson Fury au Oleksandr Usyk.

Itauma mwenye miaka 21, amepanda kwa kasi kwenye uzito wa juu, rekodi yake sio ya kitoto, katika mapambano 14, hajapoteza hata moja huku 12 kati ya hayo yakimalizika kwa kumuangusha mpinzani wake ‘KO’, inaonyesha kuwa ni balaa lingine katika ngumi za uzito wa juu.

Hali hii inaashiria mwanzo wa mabadiliko makubwa katika dunia ya ndondi, ambapo kizazi kipya kinaibuka na kuleta nguvu, mbinu na kasi ambazo hazijawahi kuonekana kabla. Mashabiki na wataalamu wanaona uwepo wa Itauma ni kama ishara ya kizazi kipya, kizazi chenye nguvu ambacho kinaweza kuibua mabadiliko makubwa kwenye uzito wa juu.

NGUM 01

SAFARI YAKE

Itauma alizaliwa Slovakia, katika mji wa Kezmarok, akiwa na baba Mnyaruka na mama Mslovaki, bondia huyo wa Kiingereza ni kaka mdogo wa bondia wa uzito wa light-heavyweight, Karol Itauma.

Familia yake ilikumbana na ubaguzi wa rangi huko Slovakia, Itauma anasema, “Mimi na ndugu zangu tuliteswa kwa rangi. Hapakuwa mahali pazuri kuwa.”

Hatimaye, familia iliamua kuhamia Uingereza, kwanza ili kuepuka mazingira ya ubaguzi wa rangi waliyoishi na pili kutafuta fursa mpya. Itauma alikuwa mtu wa mwisho wa familia kuhamia Uingereza 2008.

Wakati akikua, bondia aliyemvutia zaidi alikuwa Prince Naseem Hamed ambaye anatajwa kuwa mmoja kati ya mabondia hatari zaidi wa Kiingereza kuwahi kutokea akiwa na rekodi ya kushinda mapambano 36 kati ya 37 huku akishinda 31 kwa KO alipoteza moja tu katika maisha yake ya masumbwi.

NGUM 06

Itauma ameeleza kwamba mara zote katika upiganaji wake amekuwa akitumia ujanja wa Hamed kwenye upiganaji wake. Anasema, “Nilikuwa nikiangalia video nyingi za Naseem Hamed. Kila video ile niliitazama angalau mara 50. Alikuwa mmoja wa mabondia wangu niliowapenda zaidi. Mtindo wangu ni tofauti na wake lakini nina jaribu kuingiza baadhi ya mambo aliyoyafanya.”

Itauma alianza ndondi akiwa na umri wa miaka tisa kupitia kaka yake Karol, ambaye wakati huo alikuwa bondia wa ridhaa. Karol alimwalika kwenye gym ya ndondi siku moja na hapo ndipo alipoanza kufahamu mchezo huo. Hata hivyo, baada ya mazoezi machache magumu ya ndondi, alihama kucheza na kuamua kucheza zake soka pamoja na kaka yake mwingine, Samuel.

Baadaye, akagundua soka lingemchelewesha, akaamua kurudi zake kwenye ndondi.

NGUM 04

TAMKO LA WBO

Kufuatia ushindi wa pambano lake la 14 wikiendi iliyopita ambapo alimchapa Jermaine Franklin,  Shirikisho la Ngumu Duniani (WBO) limechukua hatua ya kihistoria kwa kumtangaza Itauma kama ‘mandatory challenger’ yani mpinzani wa lazima wa mkanda wa uzito wa juu.

Rais wa WBO, Gustavo Olivieri, alitangaza rasmi pendekezo hili akisisitiza kuwa rekodi ya Itauma pamoja na ushindi wa ‘KO’ dhidi ya Franklin, inamfanya awe staa anayestahili nafasi hiyo katika uzito wa juu.

Kama mpinzani wa lazima, Itauma atakuwa kwenye mlango wa moja kwa moja kuelekea pambano la ubingwa. Hakuna vizuizi, hakuna ucheleweshaji mrefu, hakuna mapambano madogo ya kuonesha uwezo tena.

Kwa mashabiki, hii ni ishara kuwa kizazi kipya kimeibuka, hatari mpya imeletwa ulingoni na historia inaweza kubadilika mara moja. Kwa Itauma, hii ni nafasi ya kihistoria, hatua ambayo inaweza kuunda au kubadilisha historia ya uzito wa juu wa ndondi.

NGUM 05

FURY, USYK

Kiwango cha Itauma ni changamoto mpya kwa kwa mabingwa waliopo kileleni, Fury na Usyk. Katika ndondi, kila pambano linahesabu zake.

Kwa Fury, pambano dhidi ya Itauma linaweza kuleta hatari kubwa ya kupoteza au kudhihirisha udhaifu wake huku faida ya kifedha ikiwa bado haijathibitishwa. Fury anaweza kupata mapambano yenye thamani kubwa ya kifedha dhidi ya majina makubwa kama Anthony Joshua, jambo linalofanya Itauma kuwa tishio la kibiashara kidogo kama ikitokea anapoteza.

NGUM 07

Kwa upande wa Usyk naye anaweza kujaribu kumuepuka Itauma. Anao wapinzani waliopangwa mbele yake na mpangilio wa kulinda taji lake hivyo pambano dhidi ya chipukizi kama Itauma ambaye hajajulikana kibiashara ni hatari ya kiwango cha juu. Wakubwa hawa wanapanga, wanahesabu na mara nyingi huairisha mapambano mpaka pale ambapo wataona kuna neema mbele yao.

NGUM 08

REKODI ZA FURY

Fury ambaye ni maarufu kama “Gypsy King,” ni mojawapo ya mabondia wakubwa zaidi waliowahi kuwepo katika historia ya uzito wa juu. Amejijengea jina kwa mambo matatu tofauti ikiwemo urefu, uzito na kasi katika kutupa makonde.

Fury alizaliwa Februari 12, 1988 huko Manchester, Uingereza na kuanza ndondi akiwa kijana, akiendelezwa na familia yenye historia ya ndondi. Ubora wake umefanya mashabiki na wataalamu kumtaja kama bingwa wa kihistoria, sio wa matumizi ya nguvu pake yake, bali pia kwa uwezo wa kimkakati na kiakili.

Katika rekodi yake, Fury amepigana mapambano 37, ameshinda 34, 24 kwa KO huku akipoteza mawili na kutoa sare moja.

Bondia huyo, amepewa heshima ya aina yake kwa kushinda mabondia wakubwa duniani, ikiwemo Wladimir Klitschko ambaye aliibuka bingwa wa uzito wa juu kwa muda mrefu. Ushindi huu ulikuwa mmoja wa matukio makubwa ya ndondi ya uzito wa juu katika karne hii na kuonyesha jinsi Fury alivyotumia vizuri urefu wake wa mita 2.06, nguvu na mbinu.

Mbali na ushindi wake dhidi ya Klitschko, Fury pia amepigana na mabondia wakubwa kama Deontay Wilder, Fury ameshinda mashindano haya kwa ‘KO’ moja na ushindi wa pointi nyingine, jambo lililomweka kwenye nafasi ya kihistoria ya kuwa mmoja wa mabingwa wakubwa zaidi wa uzito wa juu.

NGUM 07

REKODI ZA USYK

Usyk ni mojawapo ya mabondia wa kiwango cha juu zaidi wa kizazi chake, akijulikana kwa kasi na mbinu wakati akishambulia na kujilinda. Alizaliwa Septemba 17, 1987 nchini Ukraine na kuanza ndondi akiwa na ndoto ya kuwa bingwa wa dunia.

Kabla ya kupanda uzito wa heavyweight, Usyk alijijengea heshima kubwa katika uzito wa cruiserweight, ambapo alishinda mataji yote ya dunia, akijizolea heshima ya kimataifa kama mmoja wa mabondia bora zaidi.

Katika uzito wa cruiserweight, Usyk alishinda mapambano 18 bila kupoteza, akibadilisha historia ya ndondi ya kizazi chake. Alipata ushindi mkubwa dhidi ya mabondia waliokuwa mashuhuri duniani, akiwemo Murat Gassiev, akimalizia taji la undisputed cruiserweight world champion. Rekodi hii haikuwa tu ya ushindi ilikuwa ishara ya uwezo wake wa kiakili na kiufundi, jinsi alivyoweza kupanga mbinu zake kwa kila mpinzani na kuthibitisha hana mshindani katika uzito wake wa asili.

Baada ya kupanda uzito wa heavyweight, Usyk alikumbwa na changamoto kubwa, kupigana na mabingwa waliobobea na wenye nguvu kubwa. Hata hivyo, amepigana kwa kiwango cha juu, akishinda mapambano yote muhimu na kupata taji la WBA, WBO, IBF na IBO, akithibitisha kuwa anaweza kushinda mabingwa wa uzito wa juu zaidi bila kupoteza kasi na mbinu zake. Ushindi wake dhidi ya Anthony Joshua mwaka wa 2021 ulikuwa moja ya mapambano makubwa zaidi ya uzito wa juu.