Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyeandaa ziara ya Messi India akamatwa

MESSI Pict

Muktasari:

  • Messi kwa sasa yuko India katika sehemu yake ya ziara ya siku tatu ya ‘GOAT’ ambapo mshindi huyo mara nane wa tuzo ya Ballon d’Or anatarajiwa kuhudhuria matamasha kadhaa, kliniki za soka kwa vijana, na kufanya shughuli za hisani maeneo ya Kolkata, Hyderabad, Mumbai, na New Delhi.

KOLKATA, INDIA: MRATIBU wa ziara ya Lionel Messi nchini India amekamatwa kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano zaidi kutokana na vurugu zilizozuka wakati wa ziara ya staa huyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Salt Lake Stadium huko Kolkata.

Messi kwa sasa yuko India katika sehemu yake ya ziara ya siku tatu ya ‘GOAT’ ambapo mshindi huyo mara nane wa tuzo ya Ballon d’Or anatarajiwa kuhudhuria matamasha kadhaa, kliniki za soka kwa vijana, na kufanya shughuli za hisani maeneo ya Kolkata, Hyderabad, Mumbai, na New Delhi.

Kolkata ilikuwa kituo cha kwanza cha ziara, ambapo alikutana na mashabiki na kuzindua sanamu yake iliyopo makao makuu ya Sreebhumi Sporting Club huko Lake Town.

Messi, 38, alitembelea India kwa mara ya kwanza baada ya miaka 14, pia alionekana Salt Lake Stadium akiwa pamoja na wachezaji wenzake wa Inter Miami, Luis Suarez na Rodrigo de Paul.

Kwa muda mfupi, Messi alionekana akiwapungia mkono mashabiki waliolipa bei kubwa ya tiketi ili kumwona yeye lakini kwa bahati mbaya hakuchukua muda mrefu kiwanjani hapo na aliondolewa na walinzi mapema.

Kwa jumla, Messi alionekana kwa dakika 20 tu wakati huo mashabiki walikuwa wamelipa takribani Rupees 3,500 (Dola 38.65) ambazo ni zaidi ya nusu ya kipato cha wastani cha wiki moja cha mwananchi wa hali ya kawaida huko  India.

Baada ya Messi kuondolewa Kiwanjani, mamia ya mashabiki walijaribu kuingia uwanjani, huku wengine wakivunja viti na wakiharibu majukwaa.

“Mwisho wa tukio hili ulikuwa ni mbaya kabisa. Alikuja kwa dakika 10 tu,” amesema mshabiki mmoja kupitia The Economic Times.

 “Viongozi wote na mawaziri walikuwa wamemzunguka. Hatukuweza kuona chochote. Hakupewa hata mpira apige golini. Wamesema wangeleta Shah Rukh Khan pia. Hakuletewa mtu yeyote. Messi alikuja kwa dakika 10 na kuondoka. Pesa tulizotoa ni nyingi lakini hatujaona chochote,” amesema shabiki mwingine.

Shabiki mwingine aliyehudhuria tukio hilo amesema: “Watu wote hapa wanapenda soka. Tulitaka kumwona Messi, lakini tulikutana na udanganyifu mkubwa. Tunataka fedha zetu zirejeshwe. Usimamizi ulikuwa mbovu sana. Kolkata inajulikana kwa soka, tunapenda soka, tunaipenda Argentina, lakini tukio hili ni udanganyifu kabisa,” akaongeza. “Mawaziri walikuwa pale na watoto wao, lakini watu wengine hawakuona chochote. Tumelipishwa vibaya sana.’

Baada ya tukio hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Polisi wa West Bengal (DGP), Rajeev Kumar alithibitisha kuwa mratibu mkuu wa tukio hilo amekamatwa kwa ajili ya uchunguzi.

“Mratibu mkuu amekamatwa, uchunguzi umeanza, na tutahakikisha yeyote aliyehusika anachukuliwa hatua. Mashabiki wengi walidhani wangemuona Messi akicheza. Baadhi ya wahusika wamesema watarejesha fedha na wametoa ahadi hiyo kwa maandishi.”