Huyu Lionel Messi ana balaa kubwa!
Muktasari:
- Hilo lilikuwa taji la 47 kwa supastaa huyo wa Argentina kulinyakua kwenye maisha yake ya soka. Mshindi huyo mara nane wa Ballon d’Or aliandikisha rekodi nyingine pia ya kuwa mchezaji aliyeasisti mara nyingi kwenye historia ya mchezo wa soka, akifanya hivyo mara 405 baada ya kupiga bao la tatu la Inter Miami lililofungwa na Mateo Silvetti katika ushindi wa 5-1 dhidi ya New York City kwenye mchezo wa fainali wa Eastern Conference.
MIAMI, MAREKANI: SUPASTAA Lionel Messi amezidi kutanua rekodi yake ya kuwa mchezaji aliyebeba mataji mengi zaidi kwenye historia ya mchezo wa soka duniani baada ya kuiongoza Inter Miami kunyakua ubingwa wa Eastern Conference 2025.
Hilo lilikuwa taji la 47 kwa supastaa huyo wa Argentina kulinyakua kwenye maisha yake ya soka. Mshindi huyo mara nane wa Ballon d’Or aliandikisha rekodi nyingine pia ya kuwa mchezaji aliyeasisti mara nyingi kwenye historia ya mchezo wa soka, akifanya hivyo mara 405 baada ya kupiga bao la tatu la Inter Miami lililofungwa na Mateo Silvetti katika ushindi wa 5-1 dhidi ya New York City kwenye mchezo wa fainali wa Eastern Conference.
Lakini, kwa idadi ya mataji aliyobeba Messi, hilo ni taji dogo sana la kama Inter Miami itafanikiwa kunasa ubingwa wa Kombe la MLS. Messi bado ana mkataba Inter Miami hadi 2028, hivyo kuna nafasi kubwa ya kuendelea kubeba mataji, huku mwakani akitazamiwa kwenda kusaka taji jingine wakati Argentina itakapokwenda kujaribu kutetea taji la Kombe la Dunia 2026 katika fainali zitakazofanyika Marekani, Mexico na Canada.
Hii hapa orodha ya mataji yote aliyobeba Messi yanayomfanya supastaa huyo kuwa mchezaji aliyepamba maisha yake ya soka kwa kunyakua makombe kibao.
1.Barcelona - mataji 34
La Liga x 10: 2004–05, 2005–06, 2008–09, 2009–10, 2010–11, 2012–13, 2014–15, 2015–16, 2017–18, 2018–19
Copa del Rey x 7: 2008–09, 2011–12, 2014–15, 2015–16, 2016–17, 2017–18, 2020–21
Supercopa de Espana x 7: 2006, 2009, 2010, 2011, 2013, 2016, 2018
UEFA Champions League x 4: 2005–06, 2008–09, 2010–11, 2014–15
UEFA Super Cup x 3: 2009, 2011, 2015
FIFA Club World Cup x 3: 2009, 2011, 2015
2.PSG – mataji 3
Ligue 1 x 2: 2021–22, 2022–23
Trophee des Champions x 1: 2022
3.Inter Miami – mataji 3
Supporters’ Shield x 1: 2024
Leagues Cup x 1: 2023
Eastern Conference Title x 1: 2025
4.Argentina Under-20 – mataji 2
FIFA World Youth Championship x 1: 2005
South American U-20 Championship (Bronze): 2005
5.Argentina Under-23 – taji 1
Olympic Gold Medal x 1: 2008
6.Argentina – mataji 4
FIFA World Cup x 1: 2022
Copa America x 2: 2021, 2024
Finalissima x 1: 2022
7.Tuzo binafsi
Ballon d’Or x 8: 2009, 2010, 2011, 2012, 2015, 2019, 2021, 2023
FIFA World Player of the Year / FIFA Ballon d’Or / The Best FIFA Men’s Player x 8: 2009, 2010, 2011, 2012, 2015, 2019, 2022, 2023
European Golden Shoe x 6: 2009–10, 2011–12, 2012–13, 2016–17, 2017–18, 2018–19
FIFA World Cup Golden Ball x 2: 2014, 2022
FIFA World Cup Silver Boot x 1: 2022
FIFA Club World Cup Golden Ball x 2: 2009, 2011
FIFA U-20 World Cup Golden Ball x 1: 2005
FIFA U-20 World Cup Golden Boot x 1: 2005
UEFA Club Footballer of the Year x 1: 2008–09
UEFA Men’s Player of the Year x 2: 2010–11, 2014–15
UEFA Champions League Top Scorer x 6: 2008–09, 2009–10, 2010–11, 2011–12, 2014–15, 2018–19
Copa America Golden Ball x 2: 2015, 2021
Copa America Golden Boot x 1: 2021
La Liga Best Player x 9: 2008–09, 2009–10, 2010–11, 2011–12, 2012–13, 2014–15, 2016–17, 2017–18, 2018–19
MLS Most Valuable Player x 1: 2024
Pichichi Trophy x 8: 2009–10, 2011–12, 2012–13, 2016–17, 2017–18, 2018–19, 2019–20, 2020–21
MLS Golden Boot x 1: 2025
Laureus World Sportsman of the Year x 2: 2020, 2023
TIME Athlete of the Year x 1: 2023
IFFHS World’s Best Player x 1: 2022
Ballon d’Or Dream Team x 1: 2020
FIFPRO World XI x 17: 2007, 2008, 2009, 2010, 2011, 2012, 2013, 2014, 2015, 2016, 2017, 2018, 2019, 2020, 2021, 2022, 2023
Argentine Sportsperson of the Year x 2: 2011, 2021, 2022, 2023
Argentine Footballer of the Year x 16: 2005, 2007, 2008, 2009, 2010, 2011, 2012, 2013, 2015, 2016, 2017, 2019, 2020, 2021, 2022, 2023