Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ahadi nzito ya Paul George Celtics

AHADI Pict

Muktasari:

  • George pamoja na wachezaji wapya Mitchell Robinson na Mike Conley, ni sehemu ya jitihada za kuimarisha kikosi sambamba na Jayson Tatum ambaye ndiye mhimili mkuu wa klabu hiyo, anaingia katika msimu wake wa kwanza kamili tangu alipoumia kano Mei 2025, huku kurejea kwake mwishoni mwa msimu uliopita kukikatishwa baada ya kuondolewa katika kikosi cha Celtics kilichopoteza mchezo wa saba wa raundi ya kwanza ya mchujo dhidi Philadelphia 76ers.

BOSTON, MAREKANI: PAUL George ameweka wazi jambo moja wakati wa mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari baada ya kujiunga na Boston Celtics kwamba amesikia sauti za mashabiki ambao hawakuficha masikitiko yao kuhusu uamuzi wa uongozi wa timu hiyo kumuuza Jaylen Brown, MVP wa Fainali za NBA 2024, katika uhamisho wa Julai kwenda Philadelphia 76ers uliompeleka George kwenye timu yake ya tano katika NBA.

George, mwenye umri wa miaka 36, alisema: “Naelewa mazingira yangu. Naelewa jinsi JB alivyokuwa muhimu, si tu kwa timu hii, bali pia hapa jijini. Kwa hiyo sijachukulia jambo hili binafsi. (Mashabiki) wanapaswa kuwa na uhusiano wa kihisia na uhamisho huu.

AHA 02

“Lakini kazi yangu ni kuingia kwangu kikosini. Ni wazi kwamba miaka michache iliyopita imekuwa migumu, hasa kutokana na majeraha. Lakini binafsi najisikia vizuri. Nahisi nimevuka hatua hiyo ya kukabiliana na majeraha na sasa ninajijenga upya kwa upande wa kimwili. Na kutokana na hilo, naweza kuhamishia hali hiyo uwanjani.”

AHA 01

George pamoja na wachezaji wapya Mitchell Robinson na Mike Conley, ni sehemu ya jitihada za kuimarisha kikosi sambamba na Jayson Tatum ambaye ndiye mhimili mkuu wa klabu hiyo, anaingia katika msimu wake wa kwanza kamili tangu alipoumia kano Mei 2025, huku kurejea kwake mwishoni mwa msimu uliopita kukikatishwa baada ya kuondolewa katika kikosi cha Celtics kilichopoteza mchezo wa saba wa raundi ya kwanza ya mchujo dhidi Philadelphia 76ers.

Robinson anajiunga na Celtics akiwa ametoka kushinda ubingwa akiwa na Knicks.