AFCON 2025: Angola, Zimbabwe zagawana pointi
Muktasari:
- Dala, ambaye alifunga mara nne kwenye Afcon 2023, aliitanguza Angola akifunga bao baada ya asisti ya To Carneiro, lakini gwiji wa Zimbabwe, Musona alisawazisha mambo baada ya pasi ya Bill Antonio katika dakika za majeruhi kabla ya mapumziko.
MARRAKECH, MOROCCO: WASHAMBULIAJI Gelson Dala na Knowledge Musona kila mmoja alitupia nyavuni wakati Angola na Zimbabwe zilipogawana pointi kwenye mechi yao ya pili ya Kundi B katika mashindano ya Afcon 2025, iliyofanyika Marrakech, Ijumaa.
Dala, ambaye alifunga mara nne kwenye Afcon 2023, aliitanguza Angola akifunga bao baada ya asisti ya To Carneiro, lakini gwiji wa Zimbabwe, Musona alisawazisha mambo baada ya pasi ya Bill Antonio katika dakika za majeruhi kabla ya mapumziko.
Kipa wa Warriors, Washington Arubi alifanya kazi kubwa kwenye kipindi cha pili, alipomzuia Jonathan Buatu asifunge bao.
Mechi hiyo ilishuhudia mashambulizi ya hapa na pale huku Zimbabwe ikitegemea mashambuliaji ya mshambuliaji wao, Prince Dube, ambaye alifunga katika mechi ya kwanza. Kwa matokeo yao ya 1-1 yanazifanya Angola na Zimbabwe kukuandikisha pointi zao za kwanza kwenye Kundi B la mashindano hayo ya Afcon 2025, ambapo mechi nyingine ya kundi hilo ilishuhudia Misri ikipepetana na Afrika Kusini, ambapo zote zilishinda mechi zao za kwanza.
Katika mechi ya Angola na Zimbabwe kila timu ilipiga mashuti 11, ambapo kwa upand wa Angola sita yalilenga golini na Zimbabwe wao walilenga goli mashuti manne tu.
Lakini, ni Angola ilikuwa na mpira muda mwingi, ilipotawala kwa asilimia 63 dhidi ya 37 tu za Zimbabwe, ambaye kipa wao alifanya sevu tano kuikoa timu yake, dhidi ya tatu za kipa wa Angola, ambayo ilipiga krosi 21 dhidi ya 10 za Zimbabwe.
Timu hizo zitamaliza mechi zao za mwisho kwenye kundi hilo, kwa Angola kucheza na Misri na Zimbabwe kumalizana na Afrika Kusini, Desemba 29, 2025.