Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Achraf Hakimi akoleza mzuka Morocco ikisaka taji

HAKIMI PIct

Muktasari:

  • Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 aliyejumuishwa wiki hii kwenye kikosi bora cha FIFA cha mwaka 2025 (Best XI), alipata jeraha baada ya kuchezewa vibaya na Luis Diaz katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich jijini Paris uliopigwa Novemba.

NYOTA wa timu ya taifa ya Morocco, anayekipiga Paris Saint-Germain (PSG), Achraf Hakimi amewatia hamasa wachezaji wenzake kwa kuwataka kupambana ili kumaliza ukame wa kubeba ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) wakiwa kama wenyeji wa fainali za mwaka huu.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 aliyejumuishwa wiki hii kwenye kikosi bora cha FIFA cha mwaka 2025 (Best XI), alipata jeraha baada ya kuchezewa vibaya na Luis Diaz katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich jijini Paris uliopigwa Novemba.

Ingawa Diaz alionyeshwa kadi nyekundu, Hakimi alitolewa uwanjani akiwa na jeraha baya la kifundo cha mguu wa kushoto, hali iliyozua mashaka makubwa juu ya ushiriki wake katika fainali za AFCON.

Alipoenda kwa tabu kupokea tuzo yake wakati wa hafla ya CAF mjini Rabat, uzito wa jeraha lake ulikuwa wazi, huku akitajwa kama mmoja wa mabeki wa kulia bora zaidi duniani, Hakimi ni mhimili muhimu katika mipango ya Morocco ya kumaliza subira ya zaidi ya miaka 50 na kutwaa taji lao la pili la AFCON.

Hata hivyo, bado kuna sintofahamu juu ya lini ataweza kuivaa tena jezi nyekundu na kijani ya Atlas Lions, timu inayoongoza Afrika kwa viwango tangu ilipofika nusu fainali ya Kombe la Dunia 2022 pale Qatar.

Inaripotiwa, Hakimi aliwasili Morocco akiwa na daktari na mtaalamu wa tiba ya viungo kutoka PSG, na anaendelea na matibabu. Kuna matumaini kuwa ataweza kuanza mazoezi baadaye wiki hii.

HAKI 01

Kuna uvumi mwingi kuhusu tarehe ya kurejea kwa nyota huyo aliyewahi kuichezea Real Madrid, Borussia Dortmund na Inter Milan, kabla ya kujiunga na PSG mwaka 2021.

Kocha wa Morocco Walid Regragui amesema hataki kuhatarisha afya ya nahodha wake, jambo linaloweza kumfanya Hakimi kukosa mechi zote tatu za hatua ya makundi.

Morocco itafungua mashindano dhidi ya Comoros Jumapili, kisha itakutana na Mali tarehe 26 Desemba na Zambia siku tatu baadaye. Mechi zote zitachezwa kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdellah wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 68,000 mjini Rabat.


TISHIO ZAIDI

Mali huenda ikawa tishio kubwa zaidi, lakini ni vigumu kufikiria Morocco ikishindwa kumaliza nafasi mbili za juu na kufuzu moja kwa moja hatua ya mtoano.

Hatua ya 16 bora itaanza Januari 3, na hapo ndipo Morocco inatarajia Hakimi atakuwa tayari kucheza.

“Yeye ni kiongozi wetu, nahodha wetu,” amesema Regragui, kocha wa kwanza wa timu ya Afrika kufika nusu fainali ya Kombe la Dunia.

HAKI 02

Ingawa Morocco ni moja ya vigogo wa soka Afrika, rekodi yao ya AFCON tangu walipotwaa taji mwaka 1976 nchini Ethiopia si ya kuvutia.

Tangu ushindi huo, wamefika fainali mara moja tu, wakipoteza 2-1 dhidi ya Tunisia mwaka 2004, ambapo Regragui alikuwa beki wa kulia.

Mwaka jana waliingia AFCON Ivory Coast wakiwa vigogo wa kutwaa taji baada ya mafanikio ya Qatar, lakini walitolewa na Afrika Kusini katika hatua ya 16 bora.

Kwa sasa Morocco wako katika kiwango cha juu, wakiingia AFCON wakiwa wameshinda mechi 18 mfululizo za mashindano na kirafiki, rekodi ya dunia.

Walivunja rekodi ya Hispania Oktoba baada ya kuifunga Congo Brazzaville katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026, kisha wakashinda Mozambique na Uganda katika mechi za maandalizi ya AFCON.

HAKI 03

Ukiongeza shabiki wa Morocco ambaye ni miongoni mwa mashabiki wenye shauku na uzalendo mkubwa Afrika, si ajabu Atlas Lions wanatajwa tena kama wagombea wakuu wa taji.

Hata hivyo, kuwa mwenyeji hakuhakikishi mafanikio. Tangu mwaka 2000, ni wenyeji watatu pekee, Tunisia, Misri (2006) na Ivory Coast (2024) waliotwaa taji.

Nafasi ya Morocco kuwa mwenyeji wa nne aliyefanikiwa karne hii itaongezeka sana iwapo Hakimi atathibitishwa kuwa fiti na kuwaongoza Atlas Lions vitani.