Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Vijembe’ vya Mo Salah vyamkera Wayne Rooney, amshauri Slot

ROONEY Pict

Muktasari:

  • Kichapo hicho kimeongeza presha kubwa kwa Slot msimu huu ambao umekuwa wa kusuasua kwa Majogoo hao wa Merseyside.

GWIJI wa Manchester United, Wayne Rooney, amemshutumu nyota wa Liverpool, Mohamed Salah, akitaja tabia yake kuwa ya ubinafsi baada ya mchezaji huyo kumpiga ‘dongo’ lingine kocha wake, Arne Slot, kufuatia kichapo cha mabao 4-2 kutoka kwa Aston Villa, Ijumaa ya Mei 15, 2026.

Kichapo hicho kimeongeza presha kubwa kwa Slot msimu huu ambao umekuwa wa kusuasua kwa Majogoo hao wa Merseyside.

Liverpool kwa sasa inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa EPL, ikiwa bado haijafanikiwa kukata tiketi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya kupoteza mechi 12 kati ya 37 ilizocheza, hali inayofanya mashabiki wengi kuanza kumgeuka kocha huyo raia wa Uholanzi.

ROON 01

Salah ambaye aliingia akitokea benchi dakika za mwisho za mchezo huo baada ya kupona majeraha, anatarajiwa kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu, huku uhusiano wake na Slot ukitajwa kuingia ‘mdudu’.

Baada ya kipigo kutoka kwa Aston Villa, Salah ‘alichochea moto’ wa uhasama kwa kuandika ujumbe kwenye mitandao ya kijamii siku ya Jumamosi. 

Katika ujumbe huo, aliilaumu timu kwa ‘kusambaratika na kukubali kipigo kingine’ na kutoa wito wa kurejea kwa soka la kushambulia kwa nguvu, mtindo uliokuwa ukitumiwa na kocha aliyepita, Jurgen Klopp.

ROON 02

Akizungumza kwenye kipindi chake cha 'Wayne Rooney Show', Rooney amesema Salah amevuka mpaka na amemtaka Slot kumweka benchi au kumuacha kabisa kikosini katika mchezo wa mwisho wa kuaga kwenye Uwanja wa Anfield dhidi ya Brentford, Jumapili ijayo.

"Inasikitisha kuona haya yakitokea mwishoni mwa kile alichokifanya na kukipata ndani ya Liverpool," amesema Rooney.

"Haina maana kwake kujitokeza na kumpiga dongo lingine Slot."

Rooney aliongeza kuwa, Salah hana uwezo tena wa kucheza soka la kasi alilolisifia.

"Anataka soka la 'heavy metal', akimaanisha anataka soka la Jurgen Klopp. Mimi sidhani kama Mo Salah anaweza tena kuhimili soka la aina hiyo kwa sasa. Miguu yake imeshaishiwa nguvu ya kucheza kwa kasi na nguvu ya namna hiyo," amesema.

ROON 03

Kuhusu namna Slot anavyopaswa kushughulikia nidhamu hiyo, Rooney alitolea mfano wa maisha yake chini ya Sir Alex Ferguson huko Manchester United.

"Kama ningekuwa Arne Slot, nisingemruhusu hata kusogea karibu na uwanja katika mchezo wa mwisho. Mimi ilinitokea kwa Alex Ferguson. Tulitofautiana na kugombana, na katika mchezo wa mwisho wa Alex Ferguson pale Old Trafford, aliniacha nje ya kikosi kwa sababu hiyo hiyo," amehitimisha Rooney.

Mvutano huu unakuja ikiwa ni mwendelezo wa ugomvi wa hadharani uliotokea mapema msimu huu, ambapo Salah aliwahi kukiri wazi kuwa hana uhusiano wowote wa karibu na Slot.