Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mourinho aFUNGUKA TENA ISHU YA Pogba

Muktasari:

  • Katika siku za karibuni imeripotiwa Mourinho amekuwa na bifu na Pogba huku akimuacha nje katika mechi dhidi ya Sevilla na kumtoa katika mechi dhidi ya Newcastle, Tottenham na Bournemouth hivi majuzi.

LONDON, ENGLAND

MSINIJAZE maneno. Jana kabla ya kuanza pambano la Manchester United na Arsenal pale Old Trafford, Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho aling’aka na kudai hana bifu lolote na staa wake wa kimataifa wa Ufaransa, Paul Pogba.

Katika siku za karibuni imeripotiwa Mourinho amekuwa na bifu na Pogba huku akimuacha nje katika mechi dhidi ya Sevilla na kumtoa katika mechi dhidi ya Newcastle, Tottenham na Bournemouth hivi majuzi.

Lakini sasa Mourinho amewashutumu waandishi wa habari huku akidai hana bifu na nyota huyo kama ambavyo imekuwa ikisikika katika miezi ya karibuni huku wengine wakidai haongei kabisa na Pogba.

“Kama ingetokea miaka 10 au 15 iliyopita ingenishangaza kwa sababu nyakati hizo hakukuwa na uongo katika uandishi. Siku hizi sijui nani mwandishi nani sio mwandishi kwa sababu kila mtu anaweza kuwa mwandishi. Kiukweli mimi na Pogba hatujawahi kuwa na tatizo binafsi,” alisema Mourinho.

“Kama ukiniambia tunaweza kuwa na matatizo kwa sababu mimi kama kocha naweza kutengeneza vitu tofauti na mambo mengi, basi sawa. Lakini kwamba kuna tatizo binafsi, sio kweli. Na nina furaha kwa sababu Paul anaweza kuwa na mambo mengi, lakini kuna kitu naweza kukuhakikishia, Paul ni mpole sana,” alisema.ourinho.