Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hawa hapa ‘mabingwa’ wa sare FKF-PL

MABINGWA wa zamani Ligi Kuu Kenya, AFC Leopards, ni miongoni mwa timu sita ambazo zinaongoza kutoa sare nyingi hadi sasa msimu huu.
Timu hizo sita kila moja zimeshuhudia mechi zao 10 zikimalizika kwa sare iwe ya mabao au bila mabao.
Kabla ya FKF-PL kuchukua mapumziko ya wiki mbili, Leopards ilitoka sare ya bao 1-1 na Kenya Police FC mchezo uliopigwa Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.
Hii ilikua sare ya nne mfululizo na kocha wa Ingwe, Patrick Aussems, alikiri baada ya mchezo kuwa timu inabadilika polepole ila akafarijika kuruhusiwa kuwatumia wachezaji wanne wapya waliosajiliwa dirisha dogo mashabiki wakiamini huenda ukabadili sare hizo kuwa ushindi.
Leopards iliondokewa na takribani wachezaji 17 wengi wa kikosi cha kwanza mwanzoni mwa msimu na kumlazimu Aussems, raia wa Ubelgiji, kuwatumia zaidi wachezaji chipukizi.
Licha ya timu yake kutengeneza nafasi nyingi, tatizo likawa umaliziaji hivyo kuingia sokoni kutafuta mastraika wazoefu moja wao akiwa John Makwata aliyerudi Ingwe kwa mkopo akitokea Police FC.
Wachezaji wengine waliosajiliwa dirisha dogo na kuwapa matumaini mashabiki wa Ingwe timu itabadili sare ambazo wamezikusanya kuwa ushindi ni Cliff Nyakeya, Victor Omune na Josephat Lopaga.
“Tunasonga mbele kama kinyonga lakini haturudi nyuma,” alisema Aussems ambapo kama zile sare 10 zingekuwa ushindi, Ingwe ingekuwa na pointi 48 ikikamata nafasi ya pili pointi moja nyuma ya vinara Kakamega Homeboyz.
Timu zingine ambazo zimetoa sare michezo 10 ni Bandari FC, KCB, Police FC, Bidco United na Nzoia Sugar.