Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gor kupeleka raha FKF-PL Narok

MABINGWA wa zamani Ligi Kuu Kenya, Gor Mahia, wamepeleka mchezo wao dhidi ya Wazito FC Uwanja wa Narok katika kaunti ya Narok.
Mchezo huu awali ulikuwa upigwe jana Uwanja wa Moi jijini Kisumu lakini kamati shikilizi ya Shirikisho la Soka Kenya (FKF) ikaipeleka mbele hadi Jumamosi huku Gor Mahia ikichagua Uwanja wa Narok.
K’Ogalo imefungiwa kutumia Uwanja wa Kimataifa wa Moi Kasarani jijini Nairobi kufuatia vurugu zilizosababishwa na mashabiki wao katika mchezo wa FKF-PL dhidi ya Vihiga Bullets iliyochezwa mwezi uliopita.
Menejimenti ya Sports Stadia imeipiga marufuku Gor Mahia kutumia uwanja huo hadi itakapogharamia uharibifu wa miundombinu hivyo kuilazimu uongozi wa K’Ogalo kuchagua Uwanja wa Moi jijini Kisumu kama uwanja wa nyumbani.
Lakini ukizingatia umaarufu na wingi wa mashabiki waliyonayo Gor Mahia maarufu Sirikali, uongozi wa klabu hiyo umeamua kuwapelekea mashabiki wa soka kaunti ya Narok uhondo wa FKF-PL.
Licha ya kupeleka mchezo wao dhidi ya Wazito FC Uwanja wa Narok, kocha wa Gor Mahia, Andreas Spier, atahitaji ushindi hususan baada ya kupoteza mchezo wao wa mwisho mabao 2-0 dhidi ya Police FC.
“Nimesikitishwa kupoteza mchezo huo kwasababu hatukucheza vizuri hivyo nawaomba msamaha mashabiki,” alisema Spier.
Mbali na mechi hiyo kati ya Gor Mahia na Wazito kuhairishwa, mechi nyingine iliyopelekwa mbele ni ile kati ya AFC Leopards dhidi ya Police FC ambayo sasa itapigwa Jumapili Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.