Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

ZFF kuimarisha huduma za tiba

Muktasari:

  • Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Mipango ZFF, Awadhi Maulid Mwita katika ufunguzi wa mafunzo ya madaktari wa michezo yanayolenga kuwaongezea uwezo watendaji wa afya wanaohudumia timu za soka Zanzibar.

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) limewataka madaktari na watabibu wa timu kuongeza ujuzi katika utoaji huduma za afya ili kukabiliana na mahitaji ya kisasa kwa mpira wa miguu.

Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Mipango ZFF, Awadhi Maulid Mwita katika ufunguzi wa mafunzo ya madaktari wa michezo yanayolenga kuwaongezea uwezo watendaji wa afya wanaohudumia timu za soka Zanzibar.

Amesema ZFF inatambua mchango wa wataalamu wa afya katika maendeleo ya soka kwa sababu afya ya mchezaji ni msingi wa timu kufanya vizuri katika mashindano.

Alieleza kuwa, soka la kisasa linahitaji uwekezaji katika eneo la tiba na afya, hivyo ni vyema Zanzibar kuhakikisha wataalamu wanaohudumia timu wanapata elimu na mafunzo ya mara kwa mara.

“Baadhi ya klabu bado zinakabiliwa na changamoto za kifedha, hali inayoweza kuathiri upatikanaji wa vifaa na huduma muhimu za kitabibu, ikiwemo vifaa vya huduma ya kwanza,” amesema.

Hivyo, ZFF iko tayari kusikiliza changamoto zinazowakabili madaktari wa timu na kutafuta namna ya kuzitatua, hususani ambazo zipo ndani ya uwezo wa Shirikisho.

Aidha, amesema ZFF iko tayari kushirikiana na wadau kutafuta wadhamini kwa ajili ya kuzisaidia klabu kupata vifaa vya tiba na huduma ya kwanza ambavyo ni sehemu ya mahitaji ya msingi kwa timu.

Amesema, hatua hiyo itasaidia kupunguza mzigo kwa klabu ambazo bado zina uwezo mdogo kifedha, huku wataalamu wa afya wakipata mazingira bora ya kutekeleza majukumu yao. Awali, Mwenyekiti wa Kamati ya Tiba na Afya ZFF, Ali Ame Vuai, amesema mashirikisho ya mpira duniani yanawekeza katika wataalamu wa afya na matibabu kwa ajili ya kuhakikisha wachezaji wanapata huduma bora.

Amesema, Kamati ya Tiba na Afya imejipanga kwenda sambamba na kasi ya maendeleo ya soka duniani kwa kuhakikisha wataalamu wake wanapata mafunzo yanayowawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.