Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zandeaf yaanza na ushindi Ligi ya Viziwi

DEAF Pict

Muktasari:

  • Mabao ya washindi yalifungwa na Majaaliwa Haji dakika ya 20 na Hilmi Malik dakika 76, huku Omar Rashid akiifungia Hope City Deaf FC bao pekee dakika 40.

ZANDEAF FC imeanza vizuri mashindano ya Ligi ya Viziwi Zanzibar baada ya juzi kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Hope City Deaf FC, mechi ikichezwa kwenye Uwanja wa Mao Zedong, Unguja.

Mabao ya washindi yalifungwa na Majaaliwa Haji dakika ya 20 na Hilmi Malik dakika 76, huku Omar Rashid akiifungia Hope City Deaf FC bao pekee dakika 40.

Akizungumza baada ya mechi hiyo, Kocha Mkuu wa Zandeaf, Zuberi Zuberi amesema timu hiyo ilijitahidi kucheza katika kiwango kizuri kwa lengo la kupata ushindi na mipango yao imefanikiwa.

DE 01

Amesema licha ya kupata ushindi huo lakini bado timu haina uwanja wa kufanyia mazoezi, hivyo anaamini kama ingekuwa na uwanja mzuri wangefanya vizuri zaidi ya hivyo.

“Ligi itafungua fursa nyingi kwa upande wa viziwi na wengi wataona vipaji kutoka kwetu, nawaomba wadau wa soka kutuunga mkono kukatua changamoto zetu,” amesema Zuberi.

Naye Kocha wa Hope City Deaf FC, Rashid Yahya amesema licha ya kufungwa mchezo huo wa kwanza bado timu ilikuwa na kiwango kizuri, lakini makosa madogomadogo ndiyo yamewagharimu.

DE 02

Kocha huyo, amesema watarudi uwanja wa mazoezi kurekebisha pale ambapo kuna upunguzu lengo likiwa ni kufanya vizuri mechi ijayo kwani mwanzo umewapa mwanga wa kutambua makosa yao.

Ligi hiyo ilifunguliwa rasmi na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Zanzibar, Issa Kassim ambapo inashirikisha timu nne zinatokea Unguja itadumu kwa siku kumi hadi Septemba 27, 2026.

Lengo la kuanzishwa kwa ligi hiyo ambayo leo imeendelea kwa kuchezwa mechi moja kati ya Vuka Deaf FC na Wakombozi, ni kupata wachezaji wa timu ya taifa ya viziwi kwa ajili ya mashindano ya kimataifa yatakayofanyika nchini Ethiopia.