Z. Anto, Sholo Mwamba kusindikiza Miss na Mr Kiziwi kesho
Msanii Ally Mohamed maarufu kwa jina la Z. Anto, msanii wa kughani mashairi Mrisho Mpoto na wa singeli, Sholo Mwamba kesho wanatarajiwa kuburudisha katika fainali za kumsaka Miss na Mr Viziwi kesho.
Fainali hizo zinatarajiwa kufanyika kesho katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini humo.
Akizungumza leo Ijumaa, Oktoba 28,2022 Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo, Dk Hassan Abbasi,alisema Z. Anto atawasilisha ujumbe wa changamoto wanazopata viziwi kupitia wimbo wake 'Binti Kiziwi' ambao ni moja ya nyimbo zake zilizoanya vizuri.
Ukiachilia mbali Z. Anto aliwataja Mpoto ,msanii Sholo Mwamba na kuwahakikisha washiriki hawatajutia kuichagua Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano hayo kwa namna serikali ilivyojipanga kuwapa raha.
Akizungumzia kuhusu mashindano hayo, Dk Abbasi alisema yameiheshimisha Tanzania kwa kuwa wakati yakiwa yameanza kufanyika miaka 12 iliyopita Tanzania inakuwa nchi ya kwanza Afrika kuwa mwenyeji wake.
"Tanzania imefarijika sana kuwa wenyeji mashindano haya,kwani pamoja na mambo mengine linasaidia kuwaonyesha viziwi kuwa wanaweza kufanya kila kitu.
Akielezea namna watu watakavyoweza kushiriki Katibu huyo alisema wametoa mialiko kwa watu 1400 kati yao wakiwemo viongozi wakubwa na watu maarufu.
Hata hivyo alisema awali mgeni rasmi alitarajiwa awe Rais samia Suluhu Hassan lakini kutokana na kubanwa na majukumu atawakilishwa na Waziri wa Jinsia, Wanawake na makundi maaulum, Dk Doroth Gwajima na Waziri wa sanaa Utamaduni na Michezo, Mohamed Mchengerwa.
Pamoja na kuwepo kwa zawadi nyingine, Dk Abbasi amesema wametoa ofa ya washindi katika vipengele mbalimbali kwenda kutembelea mbuga ya Ngorongoro.
Kwa upande wake Rais wa Chama cha Viziwi Afrika, Habibu Mrope alisema dunia nzima kufika Tanzania sio jambo dogo na kuishukuru namna ambavyo imewapa ushirikiano katika kipindi kipindi chote cha maandalizi
Naye Rais wa madhindano ya viziei dunia, Bonita Annlee,amesema mashindano hayo yamesadia kuwaweka viziwi pamoja na kuonyesha dunia kuwa nao wana vipaji kama walivyo watu wa kawaida.