Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yas yashiriki Tanzania, China Nyerere Run kumuenzi Baba wa Taifa

NYERERE Pict

Muktasari:

  • Mbio hizo zilifanyika Oktoba 14, 2026 zikianzia na kuishia katika kituo cha EACLC, Ubungo jijini Dar es Salaam.

Kampuni ya mawasiliano ya Yas imeungana na washiriki wengine katika mbio za kwanza za Tanzania, China Nyerere Run 2026 kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mbio hizo zilifanyika Oktoba 14, 2026 zikianzia na kuishia katika kituo cha EACLC, Ubungo jijini Dar es Salaam.

 Mbali na kumuenzi Mwalimu Nyerere, mbio hizo zililenga kuhamasisha mazoezi kwa afya bora na kusherehekea urafiki wa kihistoria kati ya Tanzania na China.

Marathoni imekuwa ikisaidia afya kwa wakimbiaji mbalimbali pamoja na kutoa misaada mbalimbali kwa wahitaji.

Yas imekuwa ikishiriki kwenye Marathon mbalimbali kwa nia ya kuisaidia jamii hali ambayo imekuwa ikisaidia nyanja mbalimbali za jamii.

Moja ya Marathoni maarufu ambayo imekuwa ikidhaminiwa na Yas ni pamoja na Zanzibar International Marathoni ambayo mwaka huu zilihudhuriwa na zaidi ya wakimbiaji 10,000 kutoka ndani ya nje ya nchi.