Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wagombea simba wapishana TFF

WAGOMBEA Pict
WAGOMBEA Pict

Muktasari:

  • Wagombea walianza kuchukua fomu Jumatatu iliyopita, na leo ilikuwa siku ya mwisho ya kuziwasilisha baada ya kuzijaza ili mchakato wa uchaguzi uweze kuendelea.

ZOEZI la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya klabu ya Simba lilihitimishwa leo, huku wanachama kadhaa wakijitokeza katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuchukua na kurejesha fomu hizo.

Wagombea walianza kuchukua fomu Jumatatu iliyopita, na leo ilikuwa siku ya mwisho ya kuziwasilisha baada ya kuzijaza ili mchakato wa uchaguzi uweze kuendelea.

Kuanzia asubuhi hadi saa 10:30 jioni, muda ambao zoezi hilo lilitakiwa kufungwa, wanachama mbalimbali walionekana katika ofisi hizo. Baadhi walichukua na kurejesha fomu siku hiyo hiyo, huku wengine waliokuwa wamezichukua kupitia mtandao au siku zilizotangulia wakifika kuziwasilisha.


MKWABI AIBUKA TFF

Baada ya Mwanaspoti kuripoti juzi kuwa Swedi Mkwabi alikuwa amechukua fomu kupitia mtandao, leo alijitokeza katika ofisi za TFF kuirejesha.

Mkwabi alithibitisha kuwa anawania nafasi ya mwenyekiti wa klabu hiyo, akisema hakuwa na mengi ya kuzungumza kwa wakati huo kwa kuwa alikuwa akielekea kufanya maandalizi ya mchezo wa Simba dhidi ya JKT, uliopangwa kuchezwa leo.


YENGA ACHUKUA

Mwanachama wa Simba, Yusuph Omar Yenga, naye alifika ofisi za TFF leo mchana kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya ujumbe.

Yenga amesema ameamua kuingia katika kinyang’anyiro hicho kwa lengo la kuchangia mabadiliko na kusaidia kuendeleza klabu hiyo.


SASALI NAYE YUMO

Mwanachama wa Simba SC na mwandishi wa habari, Sam Sasali, leo alichukua fomu ya kuwania nafasi ya mwenyekiti wa klabu hiyo.

Sasali amesema ameamua kuwania nafasi hiyo kwa ajili ya kuleta mawazo mapya na mabadiliko ndani ya klabu.

Alieleza kuwa Simba inahitaji damu mpya na viongozi wenye mitazamo tofauti ili kukabiliana na changamoto zinazoikabili, huku akitambua na kuthamini mchango wa viongozi waliopo katika maendeleo ya timu hiyo.


JULIO AREJESHA, ACHUKUA NYINGINE

Mchezaji wa zamani wa Simba SC na Taifa Stars, Jamhuri Kihwelo, maarufu kwa jina la Julio, leo jioni alirejesha fomu ya kuwania nafasi ya ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, kabla ya kuchukua nyingine ya kuwania nafasi ya mwenyekiti wa klabu hiyo.

Julio amesema ameamua kuwania nafasi hiyo baada ya kutomuona Murtaza Mangungu, ambaye alikuwa akimsubiri hadi saa nane mchana ili achukue fomu.

Ameongeza kuwa anaamini ana uwezo wa kuiongoza Simba kutokana na historia yake ya kuitumikia klabu hiyo.