Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miquissone aanza na mkwara Singida Black Stars

JOSE Pict

Muktasari:

  • Miquissone ambaye aliwahi kuitumikia Simba na kuwa miongoni mwa wachezaji waliovutia mashabiki wa soka nchini, sasa anaanza ukurasa mpya wa maisha yake ya soka akiwa na Singida Black Stars huku akiahidi kufanya kazi kwa bidii ili kuisaidia timu hiyo kufikia malengo yake.

KIUNGO mshambuliaji wa zamani wa Simba, Luis Miquissone, amesema amefurahishwa kurejea Tanzania baada ya kujiunga na Singida Black Stars, akieleza kuwa ana kumbukumbu nyingi nzuri za nchi hii ambayo anaichukulia kama nyumbani.

Miquissone ambaye aliwahi kuitumikia Simba na kuwa miongoni mwa wachezaji waliovutia mashabiki wa soka nchini, sasa anaanza ukurasa mpya wa maisha yake ya soka akiwa na Singida Black Stars huku akiahidi kufanya kazi kwa bidii ili kuisaidia timu hiyo kufikia malengo yake.

Akizungumza baada ya kurejea nchini, nyota huyo raia wa Msumbiji amesema matarajio yake ni kutoa mchango mkubwa ndani ya kikosi hicho huku akisisitiza kuwa amekuja kufanya kazi na kuwa sehemu ya familia ya Singida Black Stars.

“Nadhani nitafanya kazi kwa bidii na kutoa kilicho bora kutoka kwangu ili kuisaidia timu. Nipo hapa kusaidia kikosi, kuwa sehemu ya timu na kufurahia soka pamoja na muda wangu hapa Tanzania,” amesema Miquissone.

Amesema kurejea kwake Tanzania kumemletea furaha kutokana na mambo mengi aliyoyakosa tangu alipoondoka, akitaja upendo wa Watanzania, utamaduni na vyakula vya hapa nchini kuwa miongoni mwa vitu vilivyomfanya atamani kurudi.

Miquissone amesema Tanzania ina nafasi ya pekee moyoni mwake kutokana na mapokezi na upendo alioupata wakati akiishi na kucheza soka nchini, akieleza kuwa anaichukulia kama nchi yake ya pili.

“Nimekosa vitu vingi kwa sababu hii ni nchi yangu ya pili. Nilipata upendo mkubwa hapa Tanzania na nimeukumbuka utamaduni, upendo wa watu na hata vyakula. Sasa nimerudi na ninafurahia kuwa hapa tena,” amesema

Kurejea kwa Miquissone kunafungua ukurasa mwingine wa safari yake ya soka nchini, ambako aliwahi kujenga jina kubwa kupitia Simba, akipata nafasi ya kuonyesha uwezo wake katika mashindano ya ndani na ya kimataifa.

Uzoefu wake wa kucheza Tanzania na mashindano ya kimataifa unaweza kuwa nyenzo muhimu kwa Singida Black Stars, ambayo inahitaji kuongeza ubora na uzoefu katika kikosi chake. Hata hivyo, matarajio ya mashabiki yatakuwa kuona namna atakavyoweza kurejesha kiwango kilichomfanya apendwe na mashabiki wa soka nchini.