Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

YAS yaendeleza udhamini wa 'Yas Kili Half International Marathon' kwa mwaka wa 13 mfululizo

MAMBIO Pict

Muktasari:

  • Aliwapongeza waandaaji, Wild Frontiers Events, pamoja na wadhamini wenza kwa kuendeleza mashindano hayo kwa miaka 25, huku akiwahimiza wakimbiaji wa ndani na nje ya nchi kujisajili mapema kupitia Mixx na kuanza maandalizi.

YAS Tanzania imethibitisha kuendelea kudhamini mbio za kilomita 21 za “Yas Kili Half Marathon” huu ukiwa ni mwaka wa 13 mfululizo. Mbio hizo ni sehemu ya Kili International Marathon zinazotarajiwa kufanyika mwakani Februari 07, 2027, mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa msimu wa 25 wa Kili International Marathon mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Mstaafu Kassim Majaliwa amesema mashindano hayo yamechangia kwa kiasi kikubwa kukuza vipaji vya wanariadha na kuitangaza Tanzania kupitia utalii wa michezo.

“Miaka 25 ni mafanikio makubwa kwa mbio hizo na yanaonyesha uthabiti, maono na ushirikiano mzuri kati ya waandaaji, wadau na Serikali ya Tanzania”, amesema Majaliwa.

Ameongeza kuwa mbio hizo zimewapa wanariadha wa Tanzania nafasi ya kujipima na kupata uzoefu wa kushindana na wakimbiaji kutoka mataifa mbalimbali. Aliwataka wadau kuendelea kuwasaidia wanariadha wa ndani ili kuongeza ushindani wao katika mashindano makubwa.

Majaliwa pia amesema ujio wa mbio hizo unachochea uchumi wa Tanzania na kutoa fursa kwa wafanyabiashara mbalimbali mkoani Kilimanjaro na maeneo ya jirani kuingiza kipato. Aliwahimiza washiriki kuwa licha ya kukimbia basi watumie fursa  hiyo kutembelea vivutio vya utalii vinavyopatikana mkoani Kilimanjaro.

Kwa upande wake, Meneja wa Chapa na Mawasiliano- Yas Tanzania, Woinde Shisael, amesema, “Tunajivunia kuendelea kuwa sehemu ya mbio hizi kwa mwaka wa 13 mfululizo kutokana na mchango wake katika kuhamasisha afya, kukuza utalii wa michezo na vipaji vya wanariadha, pamoja na kuleta fursa za kiuchumi kwa wakazi wa Moshi na Tanzania kwa ujumla,”

Amesema kaulimbiu ya Yas mwaka huu “Mbio za Viwango hadi kileleni” inawahakikishia washiriki wote kupata uzoefu (experience) yenye viwango vya kimataifa huku wakifurahia mtandao swadakta wa viwango. Kauli  mbiu hii, inaenda sambamba na utambulisho mpya wa mtandao wetu ‘Mtandao wa Viwango’ baada ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na Kampuni ili kuboresha huduma za mawasiliano.

“Washiriki wanahitaji mtandao wenye kasi na unaopatikana kwa uhakika ili kuendelea kuwasiliana na familia na marafiki, pamoja na kufuatilia shughuli zao mbalimbali wakiwa Moshi. Kupitia Mtandao wa Viwango, tumejipanga kuwawezesha kufanya hayo huku wakifurahia mbio hizi,” amesema.

Shisael amesema kampuni hiyo pia itaendeleza utamaduni wake wa upandaji miti kando kando ya mlima Kilimanjaro na kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira ili kusaidia kulinda ikolojia na uoto wa Mlima Kilimanjaro.

“Mwaka jana tulifanikiwa kupanda miti zaidi ya 65,000 na kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa wanajamii, wakiwemo wanafunzi. Tutaendelea na utamaduni huu katika mbio za mwaka 2027,” amesema.

Aliwapongeza waandaaji, Wild Frontiers Events, pamoja na wadhamini wenza kwa kuendeleza mashindano hayo kwa miaka 25, huku akiwahimiza wakimbiaji wa ndani na nje ya nchi kujisajili mapema kupitia Mixx na kuanza maandalizi.