Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kivelege atoa zawadi ya mabao Mlandege

KIVELEGE Pict

Muktasari:

  • Kivelege alikuwa nyota wa mchezo huo wa Ligi Kuu Zanzibar ambapo Mlandege iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mwenge.

MSHAMBULIAJI wa Mlandege, Boniphace Kivelege amesema mabao mawili aliyofunga dhidi ya Mwenge ni zawadi maalumu kwa mashabiki na uongozi kutokana na mchango wao katika kuisukuma timu hiyo kupata matokeo mazuri.

Kivelege alikuwa nyota wa mchezo huo wa Ligi Kuu Zanzibar ambapo Mlandege iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mwenge.

Akizungumza baada ya mchezo huo, mshambuliaji huyo amesema ameamua kulitenga bao moja kwa ajili ya mashabiki na wapenzi wa Mlandege, huku la pili likiwa ni zawadi kwa uongozi wa klabu hiyo kama ishara ya kuthamini mchango wao.

Amesema uamuzi huo umetokana na namna mashabiki na viongozi walivyoendelea kuipa timu sapoti licha ya kupitia kipindi kigumu cha matokeo katika michezo iliyopita ya ligi.

“Ushindi dhidi ya Mwenge SC umerejesha motisha na hali nzuri ndani ya timu. Hilo linanipa nguvu zaidi ya kufanya vizuri katika michezo ijayo,” amesema Kivelege.

Ameongeza kuwa kwa sasa ameanza kuona mwelekeo mzuri wa timu hiyo, jambo linalowapa hamasa ya kuendelea kupambana ili kupata matokeo mazuri katika michezo inayofuata.

Ushindi huo umeifanya Mlandege kupanda hadi nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 14 baada ya kucheza michezo 12, huku Mwenge SC ikibaki nafasi ya 15 ikiwa na pointi sita katika michezo 12.

Katika michezo mingine, Zimamoto iliendelea kuongoza ligi ikiwa na pointi 31 baada ya kuichapa Fufuni mabao 2-1. Wembe SC iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mafunzo SC, huku Chipukizi United ikiifunga KMKM SC mabao 2-1.