Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yaweka historia CAF ikitinga makundi mara tano mfululizo

Picha na Mtandao

Yanga imeandika historia ya kufuzu hatua ya makundi kwa mara ya tano mfululizo baada ya kuitandika CFFA ya Madagascar kwa mabao 4-1 katika mechi iliyochezwa leo Jumatano, Oktoba 21, 2026 katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Yanga ilianza kupata bao katika dakika ya 27 baada ya beki wa kulia, Ibrahim Kazimoto kumalizia kwa kichwa kona iliyochongwa na Mudathir Yahya, mabao mengine mawili yalifungwa na Selemani Mwalimu katika dakika ya 49 na 53 na lile la Juma Abushiri alilofunga dakika ya 82.

Ushindi huo umeifanya Yanga itinge makundi kwa jumla ya mabao 8-1 baada ya mechi ya kwanza ugenini kushinda mabao 4-0.

YANG 01

Historia hiyo ilianza kuandikwa msimu wa 2022/2023 wakati Yanga ilipotinga hatua ya makundi kabla ya kuweka rekodi ya kucheza hadi Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Baada ya mafanikio hayo, Yanga ilirejea kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Afrika katika msimu wa 2023/2024 na kufanikiwa tena kutinga atua ya Makundi, kabla ya kwenda mbali zaidi na kutinga robo fainali ilipotolewa na Mamelodi Sundown kwa mikwaju ya penati 4-2 kufuatia suluhu.

YANG 02

Msimu wa 2024/2025 kikosi hicho kilichokuwa chini ya kocha Miguel Gamondi kiliendeleza mafanikio hayo  kwa kutinga tena Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na msimu uliopita ilipocheza tena hatua hiyo.

YANG 03

Leo hii, Oktoba 21, 2026, msimu wa 2026/2027 unashuhudia historia mpya ikiandikwa kwa mara ya tano mfululizo baada ya kuisambaratisha CFFA ya Madagascar na jumla ya mabao 8-1 na kukata tiketi ya makundi kwa kishindo.