Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yawakumbuka waliokosa tiketi

SKRINI Pict

Muktasari:

  • Huu ni mtindo wa tofauti na ule uliokuwa jana Jumamosi katika Tamasha la Simba Day ambapo mashabiki hawakupata Nafasi ya kutazama mechi hiyo nje ya uwanja kwa wale ambao walikosa nafasi ya kuingia ndani.

YANGA imekuja tofauti kwa kuwawekea viti na screen kubwa nje ya Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaa ili mashabiki ambao watahudhuria Tamasha la Yanga Day na kukosa nafasi ya kuingia ndani, washuhudie matukio kwa nje.

Huu ni mtindo wa tofauti na ule uliokuwa jana Jumamosi katika Tamasha la Simba Day ambapo mashabiki hawakupata Nafasi ya kutazama mechi hiyo nje ya uwanja kwa wale ambao walikosa nafasi ya kuingia ndani.

Uwanja wa Uhuru una uwezo wa kuingiza watazamaji 19,000 waliokaa, hivyo mashabiki watakaotamani kuona matukio yote mubashara na wamekosa tiketi ya kuingia ndani, hii ni fursa nzuri kwao.

Katika Tamasha la Yanga Day linalofanyika leo Jumapili Agosti 9, 2026, mashabiki wa timu hiyo mbali na kushuhudia burudani mbalimbali, pia watashuhudia kikosi chao kitakachoshiriki mashindano ya msimu ujao 2026-2027.

Hivi sasa kuna shughuli mbali mbali zinazoendelea, huku mashabiki wakizidi kusogea maeneo ya uwanja taratibu na burudani ya muziki ikisikika kutokea ndani ya uwanja.