Yanga yatesti mitambo, yampiga mtu wiki
Muktasari:
- Katika mchezo huo mabao ya Yanga yamefungwa na Chadrack Boka akipokea asisti ya Maxi Nzengeli, Albert Kangwanda akitengenezewa na Cheikh Toure.
Yanga imecheza mchezo wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Magereza ya Dar es Salaam ikishinda kwa mabao 7-2.
Mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa mazoezi wa timu hiyo wa Avic, Yanga imetumia karibu wachezaji wake wote walioingia kambini kujiandaa na msimu mpya.
Katika mchezo huo mabao ya Yanga yamefungwa na Chadrack Boka akipokea asisti ya Maxi Nzengeli, Albert Kangwanda akitengenezewa na Cheikh Toure.
Mabao mengine yamefungwa na Laurindo Aurelio 'Depu' aliyefunga mara mbili akitumia asisti ya Allan Okello, Edmund John, Okello na Abdulnassir Mohammed 'Casemiro'.
Kocha wa Yanga, Manqoba Mngqithi ametumia mchezo huo kupima mazoezi ya wachezaji wake yaliyofanyika kwa wiki mbili sasa.
Yanga imekuwa ikifanya mazoezi makali ikitumia saa nne ikiendelea kujipanga na hesabu za msimu mpya.
Inaelezwa kwa ratiba ya Mngqithi kikosi hicho kitakuwa kila baada ya mazoezi ya siku saba kitacheza mchezo wa kirafiki kupima kiwango cha utimamu wa kile walichojifunza wachezaji.