Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yajifungia CCM Liti

Mashabiki wakiwa juu ya kontena lililopo nje ya Uwanja wa Liti mkoani Singida wakati Yanga wakifanya mazoezi ndani ya uwanja

Yanga imefanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa CCM Liti mkoani Singida huku makomandoo wake wakizuia waandishi na hata mashabiki kuhudhuria mazoezi hayo.

Yanga ambayo kesho Mei 4 itacheza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya wenyeji wao Singida Big Stars ilitua Uwanja huo 9:50 alasiri tayari kwa mazoezi hayo huku walinzi wao maarufu kwa jina la Makomandoo wakiwa wameuzunguka Uwanja huo ndani na nje.

Ndani ya uwanja huo hakukuwa na ruhusa ya kupiga picha yoyote kuanzia timu hiyo ilipoingia na hata ilipokuwa inafanya mazoezi yake yaliyochukua saa 1:20.

Huku nje ya uwanja kiu ya mashabiki wa Yanga waliotaka kuangalia timu yao ilishindikana kutibiwa kwa zuio hilo huku wakitulizwa kwa kuambiwa wataiona kesho uwanjani wakati ikicheza mechi.

Katika mazoezi hayo Yanga ikiwakosa Dickson Ambundo na beki David Bryson pekee kikosi chao kimefanya mazoezi makali ya mbinu kuelekea mechi hiyo.

Kikosi hicho kilionekana kuwa na morali katika mazoezi yake yakisimamiwa na makocha wao Nasreddine Nabi na wasaidizi wake Cedric Kaze, Khalil Ben Youssef na kocha wa makipa Milton Nienov.

Yanga ambayo ndio kinara kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 68 itashuka kwenye Uwanja wa Liti kutafuta alama tatu zitakazowasaidia kulisogelea taji lao la ubingwa wanaoushikilia  huku Singida wenye alama 51 wakiwa nafasi ya nne wao wakihitaji alama kama hizo zitakazowasaidia kuendelea kuwakimbiza Azam wenye alama 53 katika kuwania nafasi ya tatu kwenye msimamo.