Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yaitangulia Simba fainali Mapinduzi

Ngoma ya kuamua nani acheze fainali za Kombe la Mapinduzi baina ya Yanga na Azam Fc ilikuwa ngumu hadi baada ya kuingia kwenye mikwaju ya penati kwani dakika 90 za awali timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

Yanga wametinga fainali hizo kwa penalti 5-4 ambapo sasa itamsubiri mshindi kati ya Simba na Namungo mechi itayochezwa saa 2:15 usiku.

Penati za Yanga kwa waliopata zilifungwa na Tuisila Kisinda, Mukoko Tonombe, Paul Godfrey, Abdallah Shaibu na Zawadi Mauya wakati Michael Sarpong akikosa penati ya kwanza kabisa.

Upande wa Azam nyota wao wawili walikosa penati hizo ambao ni Awesu Awesu na Daniel Amour huku Bruce Kangwa, Ally Niyonzima, Mudathir Yahya na Wadada wakipata.

Katika mchezo huo nyota wa Yanga Yacouba Songne alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia hivyo kocha Cedric Kaze alilazimika kufanya mabadiliko kwa kumuingiza Abdulkarim Yunus.

Yacouba aliumia kipindi cha kwanza cha mechi hiyo dhidi ya Azam FC ambapo timu hizo zilikwenda mapumziko zikiwa hazijafungana, mechi hiyo ilikuwa ni ya nusu fainali ya kwanza ya Kombe la Mapinduzi ambayo fainali zake ni keshokutwa Jumatano.

Yacouba aliumia wakati wanagombania mpira langoni mwa Azam Fc ambapo alipata matibabu na kuendelea kucheza lakini dakika ya 42 alishindwa kuendelea na mchezo kwani alionekana kuwa na maumivu.

Daktari wa Yanga Shecky Mngazija alipompa huduma ya kwanza alionekana kuamuru mchezaji huyo asiendelee na mchezo ndipo mabadiliko yalifanyika.

Katika kipindi cha kwanza timu hizo zilicheza kwa kushambuliana kwa zamu huku kila upande ukishindwa kuzitumia nafasi walizokuwa wanazipata.

Dakika ya nne, Mshambuliaji wa Yanga Michael Sarpong alikosa bao la wazi baada ya kupiga shuti lililitoka nje ya goli huku mwamuzi wa mchezo huo Rashid Farahan Issa akimpa kadi ya njani mchezaji wa Azam Bruce Kangwa dakika ya 26 kwa kucheza rafu.

Dakika ya 26, Yacouba aliyeonekana nyota wa Yanga kwa kipindi cha kwanza alikosa bao baada ya kupiga mpira nje kidogo ya goli akiwa amezongwa na wachezaji wa Azam Fc.

Obrey Chirwa alijibu mapigo dakika ya 32 naye alikosa bao kwani shuti lake alipiga lilipaa juu ya goli akiwa yeye na kipa Farouk Shikalo.

Kipindi cha pili timu hizo ziliingia kwa kasi huku zikiendelea kushambuliana kwa zamu ambapo Tuisila Kisinda aliipatia Yanga bao la kuongoza dakika ya 52 akiwazidi kasi mabeki wa Azam huku kipa wao Wilbol Changarawe akishindwa namna ya kuokoa mpira huo huku Kisinda akikosa tena bao la wazi dakika ya 56.

Hata hivyo, Shikhalo alishindwa kuisadia timu yako isisawazishiwe bao dakika ya 66 lililofungwa na Obrey Chirwa baada ya kujaribu kutoka golini huku mabeki wake nao wakipambana namna ya kuzuia lakini walijikuta wanampa nafasi Chirwa ya  kufunga bao kirahisi.

Makocha wote wawili walifanya mabadiliko kipindi cha pili ambapo George Lwandamina wa Azam FC aliwatoa Never  Tigere, Mpiana Monzinzi, Salum Abubakar 'Sure Boy', Frank Domayo na kipa Changarawe nafasi zao zilichukuliwa na Awesu Awesu, Emma Kebelege, Ally Niyonzima,  Mudathir Yahaya na Benedict Haule.

Kocha wa Yanga, Kaze aliwatoa Yacouba aliingia Yunus, Adeyun Saleh nafasi yake ilichukuliwa na Paul Godfrey 'Boxer'.

Katika mchezo huo kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima alitangazwa mchezaji bora wa nusu fainali hiyo ambapo alizawadiwa Sh 500,000 pesa ambayo ni mabadiliko na awali ambapo walikuwa wakipewa Sh 200,000.

Yanga: Farouk Shikalo, Kibwana Shomari, Adeyum Saleh, Said Makapu, Abdallah Shaibu, Mukoko Tonombe, Tuisila Kisinda, Zawadi Mauya, Michael Sarpong, Haruna Niyonzima na Yacouba Songen.

Azam FC: Wilbol Changarawe, Nico Wadada, Bruce Kangwe, Daniel Amoah, Abdallah Kheri, Frank Domayo, Obrey Chirwa, Salum Abubakary, Mpiana Monzinzi, Never Tigere na Iddi Nado.