Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga inaanza safari ya ubingwa

YANGA Pict

Muktasari:

  • Mstari wa mbele wa Yanga umeonekana kuwa ndio idara tishio zaidi kwa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu kutokana na takwimu bora na muendelezo mzuri wa kufumania nyavu ambao umekuwa nao katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

SAFU ya ulinzi ya Namungo leo inalazimika kuwa katika kiwango bora na kucheza kwa nidhamu kubwa dhidi ya Yanga ili iondoke na pointi nyumbani katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Tanzania Bara baina ya timu hizo msimu huu kwenye Uwanja wa Majaliwa Ruangwa Lindi kuanzia saa 3:00 usiku.

Mstari wa mbele wa Yanga umeonekana kuwa ndio idara tishio zaidi kwa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu kutokana na takwimu bora na muendelezo mzuri wa kufumania nyavu ambao umekuwa nao katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

YANG 01

Kumbukumbu zinaonyesha, Yanga imefunga bao katika michezo 15 mfululizo ya Ligi Kuu ya NBC na mara ya mwisho kuondoka bila kufumania nyavu ilikuwa ni Machi 18, mwaka huu iipolazimishwa sare tasa na TRA United.

Katika mechi hizo 15 mfululizo ambazo safu ya ushambuliaji ya Yanga ilifumania nyavu, timu hiyo imepachika idadi ya mabao 40 ikiwa ni wastani wa mabao 2.7.

YANG 02

Wakati ikifunga mabao hayo 40, Yanga imeruhusu nyavu zake kutikiswa mara sita tu katika mechi hizo 15 zilizopita za Ligi Kuu.

Namungo imekuwa na mwenendo mzuri wa kuruhusu mabao mara kwa mara na kuthibitisha hilo, katika mechi 12 zilizopita za Ligi Kuu, imefungwa mabao 13 ikiwa ni wastani wa bao moja kwa mechi. Timu hiyo inayonolewa na Kocha Juma Mgunda, katika mechi hizo 12 zilizopita, imefunga mabao tisa tu ikiwa ni wastani wa bao 0.8 kwa mechi.

YANG 03

Mechi hiyo itatanguliwa na mchezo wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha baina ya Polisi Tanzania na Azam FC kuanzia saa 10:00 jioni. Katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Coastal Union wataikaribisha Mashujaa kuanza saa 12:30 jioni.