Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Okello, Aziz KI: Mambo yako hivi Yanga

OKELLO Pict


KUNA uwezekano katika kikosi cha Yanga kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili Agosti 15, 2026 kikawa na mabadiliko ya wachezaji wanaoingia na kutoka kama ambavyo Mwanaspoti lilivyopata taarifa za ndani.


Zipo taarifa za ndani ya Yanga zinazosema kwamba, klabu hiyo imepokea ofa ya Sh2 bilioni kutoka Wydad Casablanca na AS FAR Rabat zote za Morocco zikimtaka kiungo mshambuliaji, Allan Okello ambaye msimu uliopita alicheza kwa kiwango cha juu akitua Yanga dirisha dogo la Januari 2026, akifunga mabao 14 na asisti nane za Ligi Kuu.


Wakati Yanga ikiwa na ofa ya kumuuza Okello, inataka kumaliza dirisha la usajili kwa kumuongeza kiungo mshambuliaji, Stephanie Aziz KI kwenye kikosi chao.

Aziz KI amefanikiwa kumalizana na klabu yake ya Libya baada ya Yanga kulipa pesa ambazo zilikuwa zinahitajika ili aweze kurejea klabuni hapo.

OKE 01

Meneja wa Aziz KI, Zambro Traore, alishawasili nchini kuanzia juzi kwa ajili ya kumaliza dili hilo na Yanga ambapo wakati wowote atasaini mkataba wa miaka miwili.

Juzi Aziz KI alikuwa jukwaani kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar pamoja na meneja wake huyo kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii ambapo Yanga iliifunga Simba bao 1-0 ambapo usiku wake walionekana kuwa na mabosi wa Yanga wakipata chakula cha pamoja.

Yanga imethibitisha kupokea ofa kwa ajili ya kumuuza Okello, ambapo Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ally Kamwe amesema: "Tumepokea hizo ofa ni kweli lakini uongozi bado haujafanya uamuzi wowote, tunataka kupima kile ambacho kitakuwa sahihi kwetu kulingana na thamani ya mchezaji wetu.”

Yanga inataka kama itamuuza Okello basi nafasi yake ichukuliwe na Aziz KI, lakini hesabu zingine ni kwamba kama dili hilo la Okello likikwama kuna uwezekano wa kumuondoa beki wake mpya, Farouk Komara kutokana na bado hajawashawishi sana.

OKE 02
OKE 02

Aziz KI anakumbukwa zaidi ndani ya Yanga kwa muda wa misimu mitatu aliyocheza hapo akitokea ASEC Mimosas ya Ivory Coast, ambapo msimu wa 2023-2024 aliibuka kinara wa ufungaji Ligi Kuu Bara akipachika mabao 21 na asisti nane, aliondoka mwisho wa msimu wa 2024-2025 kujiunga na Wydad Casablanca ya Morocco.

Ndani ya Wydad, hakudumu sana kwani alicheza hadi Januari 2026 akajiunga na Al-Ittihad Tripoli ya Libya ambapo baada ya hapo zikaibuka tetesi za kurejea Yanga.

Kama Yanga itamuuza Okello aliyefunga mabao 14 ya Ligi Kuu Bara, basi itakuwa imeondoa jumla ya mabao 33 ya Ligi Kuu Bara yaliyopatikana msimu uliopita ambapo 10 yalifungwa na Prince Dube aliyekwenda Hardrock FC ya kwao Zimbabwe na mabao tisa ya Laurindo Dilson 'Depu' aliyeuzwa Petro Atletico de Luanda ya kwao Angola.