Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wydad yamrudisha Mwalimu Morocco

Muktasari:

  • Chanzo kutoka ndani ya Simba kimeliambia Mwanaspoti kuwa, mkataba wa mkopo wa Mwalimu kutoka Wydad Athletic Club ulimalizika baada ya msimu uliopita 2025-2026, hivyo kwa taratibu za usajili alitakiwa kurejea Morocco kuripoti kwa waajiri wake kabla ya hatua nyingine yoyote kuchukuliwa.

KIGALI: TAARIFA kutoka hapa Rwanda zinabainisha kwamba, mshambuliaji wa Simba, Seleman Mwalimu ameondoka na kurejea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya utaratibu wa kwenda Morocco kuungana na kikosi cha Wydad Athletic kufuatia mkataba wake wa mkopo na Wekundu wa Msimbazi kumalizika.

Chanzo kutoka ndani ya Simba kimeliambia Mwanaspoti kuwa, mkataba wa mkopo wa Mwalimu kutoka Wydad Athletic Club ulimalizika baada ya msimu uliopita 2025-2026, hivyo kwa taratibu za usajili alitakiwa kurejea Morocco kuripoti kwa waajiri wake kabla ya hatua nyingine yoyote kuchukuliwa.

Mtoa taarifa huyo aliendelea kueleza kwamba, Simba ilikuwa na nia ya kuendelea kubaki na mchezaji huyo kwa mkopo wa msimu mwingine, lakini mchakato huo ulipaswa kuanza baada ya Mwalimu kuripoti Wydad na kujiunga na maandalizi ya msimu mpya na sio kama ilivyofanyika kwa nyota huyo kuendelea kusalia Msimbazi.

"Hakuna mgogoro kati ya Simba na Wydad. Kilichopo ni kufuata utaratibu unaotakiwa. Mchezaji anatakiwa kwanza arudi kwenye klabu yake, kocha mpya amuone, ndipo mazungumzo yaendelee. Simba bado ina nia ya kumbakiza, lakini uamuzi haupo upande mmoja pekee," kilisema chanzo hicho.

Inaelezwa kuwa benchi jipya la ufundi la Wydad chini ya kocha raia wa Ureno, Paulo Sergio, linataka kwanza kumuona Mwalimu katika maandalizi kabla ya kufanya uamuzi wa kama ataendelea kubaki kikosini, atatolewa tena kwa mkopo au klabu itaamua kufanya biashara kwa kumuuza.

Tofauti na taarifa zilizozagaa zikidai Simba ilikuwa tayari imekamilisha kila kitu kuhusu Mwalimu hadi kufikia uamuzi wa klabu hiyo kutangaza, ukweli ni kwamba mazungumzo bado yanaendelea na uamuzi wa mwisho utategemea pia tathmini ya benchi jipya la Wydad.

Mfano unaotolewa ndani ya Simba ni ule wa kiungo raia wa Afrika Kusini, Neo Maema ambaye baada ya mkataba wake wa mkopo kumalizika, klabu hiyo iliomba ruhusa maalumu kutoka Mamelodi Sundowns ili aendelee kucheza mchezo mmoja wa mwisho wa Kombe la CRDB dhidi ya Azam uliofanyika Julai 4, 2026.

Baada ya ruhusa hiyo kutolewa, Maema aliichezea Simba mechi hiyo kabla ya kurejea Afrika Kusini kuripoti kwa klabu yake ya Mamelodi kama taratibu zinavyotaka. Baada ya hapo ndipo Simba ilianza mazungumzo mapya ya kutaka kumbakiza.

"Kwa sasa jambo la muhimu ni kusubiri hatua za Wydad baada ya maandalizi kuanza. Simba inaendelea na mazungumzo, lakini hatuwezi kusema kila kitu kimekamilika wakati mchakato bado unaendelea," kimeongeza chanzo hicho.

Kwa sasa Wekundu wa Msimbazi wanaendelea na maandalizi kupitia michuano ya CECAFA Kagame nchini Rwanda, wakijiandaa na mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Singida Black Stars utakaochezwa Ijumaa Julai 31, 2026.