Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtihani wa Kassali Simba

Muktasari:

  • Kassali ana kazi mbele yake ya kujitengenezea ufalme kama ilivyokuwa kwa makipa waliofanikiwa kuwa vipenzi vya mashabiki wa Wanamsimbazi, kutokana na kazi zao.

KITENDAWILI kinachomsubiri akitegue golikipa wa Simba, Mahamadou Kassali msimu unaotarajiwa kuanza Agosti 14, 2026 ni ushawishi wake wa kufanya kazi nzuri itakayowafurahisha viongozi na mashabiki wa timu hiyo.

Kassali ana kazi mbele yake ya kujitengenezea ufalme kama ilivyokuwa kwa makipa waliofanikiwa kuwa vipenzi vya mashabiki wa Wanamsimbazi, kutokana na kazi zao.

Siyo kwamba msimu uliopita wa 2025-2026 Kassali hakufanya vizuri, isipokuwa kazi yake golini iwe na nguvu mbele ya mashabiki kama ilivyokuwa kwa watangulizi wake.

Msimu wa 2022-2023, Aishi Manula alimaliza na cleansheets 12 akiwa namba mbili nyuma ya kipa wa Yanga, Djigui Diar-ra aliyekuwa na 17.

Manula alipoumia msimu wa 2023-2024, ndipo dirisha dogo Simba ilipomsajili golikipa Ayoub Lakred ambaye kwa sasa anacheza FUS Rabat ya nchini kwao Morocco.

Kiwango cha Lakred kiliwaondoa wasiwasi mashabiki wa Simba kuamini golini kuna mtu sahihi anayeweza kufanya ma-kubwa kama ilivyokuwa imezoeleka kwa Manula.

Baada ya Lakred kuumia, Simba ilimtoa kwenye mfumo wa usajili msimu wa 2024-2025 akasajiliwa golikipa Moussa Ca-mara ambaye alipafomu kwa kiwango cha juu kiasi cha msimu wake wa kwanza huo alimaliza kinara wa cleansheet akikusanya 19 na kuvunja rekodi ya Manula aliyokuwa ameandika 2017-2018.

Baada ya Camara kuumia msimu uliopita wa 2025-2026, alitolewa katika mfumo wa usajili akasajiliwa Kassali akitokea AS FAN ya nchini Niger akiingia dirisha dogo, akamaliza nafasi ya pili kwa cleansheets zake 16 katika ligi, kinara akiwa Diarra aliyekuwa na 18, hivyo atakachokifanya msimu ujao kinaweza kumpa sifa zaidi au kumshusha.

Kutokana na mtihani unaomkabili kipa huyo ambaye Simba imemuamini kuendelea naye msimu ujao wa 2026-2027, aliyekuwa kocha wa makipa wa klabu hiyo, Idd Pazi alisema: “Alichokuwa amefanikiwa Camara alifanya vizuri ndani ya muda mfupi, ni kati ya makipa waliokuwa wanajiamini golini, hilo lilipunguza washambuliaji wa timu pinzani kujiamini kama ilivyo kwa Diarra, hivyo anachotakiwa kufanya Kassali ni uwezo wake uwashawishi mashabiki.”

Mwingine aliyechangia hilo ni kipa wa zamani wa Yanga, Benjamin Haule, aliyesema: “Kassali ni kipa mzuri ila anatakiwa apambane zaidi, kazi ya soka inafanyika peupe, akifikia kiwango cha kuwashawishi mashabiki watamuimba tu.”

Aliongeza: “Katika klabu ya Simba kumepita makipa wengi waliokuwa Tanzania One kama Juma Kaseja, Manula lakini kila mmoja alipata ufalme wake kulingana na huduma yake, pia kwa wageni Camara alionyesha ushindani hata mechi za dabi zikikutana Simba na Yanga unaangalia makipa unaona kuna kitu watakifanya.”