Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

WPL kuna viporo vitatu vinaliwa leo

Muktasari:

  • Viporo vitatu vya raundi ya kwanza vilipigwa Desemba 8, Alliance Girls iliondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Fountain Gate Princess, mechi ya JKT vs Bunda Queens, Tausi FC na Mashujaa Queens hazikuchezwa baada ya wapinzani kutotokea uwanjani.

LIGI Kuu ya Wanawake (WPL), inatarajiwa kuendelea tena kwa kupigwa mechi tatu za viporo zitakazopigwa leo kwenye viwanja vitatu tofauti ikiwemo moja ya JKT Queens dhidi ya Bilo Queens.

Viporo vitatu vya raundi ya kwanza vilipigwa Desemba 8, Alliance Girls iliondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Fountain Gate Princess, mechi ya JKT vs Bunda Queens, Tausi FC na Mashujaa Queens hazikuchezwa baada ya wapinzani kutotokea uwanjani.

Raundi ya pili JKT itamkaribisha Bilo ambao ni mara yao ya kwanza kushiriki ligi mechi itakayopigwa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Tausi v Yanga Princess (KMC Complex) na Ruangwa Queens v Mashujaa (CCM Majaliwa Lindi).

Akizungumzia mechi hiyo, nahodha wa Mashujaa, Sabina Emmanuel alisema wanafahamu umuhimu wa mechi hiyo na kwamba watapambana kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu licha ya ugumu wa mechi hiyo.

“Hatujawahi kucheza na Ruangwa ndio mara ya kwanza kucheza ligi hivyo ni ngumu kujua wanatumia mbinu gani na unaona ni ngumu kiasi gani kucheza na timu ambayo huifahamu vizuri lakini kama wachezaji tumejipanga kuhakikisha mbinu za kocha tunazifuata vizuri,” alisema Sabina.

Nahodha wa JKT Queens, Anastazia Katunzi alisema lengo la kwanza ni kupambania pointi tatu kila mechi ili waweze kurejesha taji hilo akikiri haitakuwa rahisi kutokana na ubora wa wapinzani wanaokutana nao.

“Ligi imekua sasa hivi usipojipanga na kuchanga vizuri karata zako unaweza kudondosha pointi hata ukiwa nyumbani kwa hiyo kama wachezaji tuko makini na tunaamini tutapambana kila hatua kuhakikisha jambo linakwenda sawa msimu huu.”

Katika mechi ya kwanza ya kiporo tangu irudi kutoka katika Fainali za Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake iliyofanyika Misri, JKT Queens ilitakiwa kuvaana na Bunda Queens lakini wapinzani wao hao hawakutokea uwanjani na kuwaweka watetezi hao wa WPL nafasi ya kuzoa pointi za dezo.

Hata hivyo, uamuzi kamili ya mechi hiyo na ile ya Tausi FC na Yanga Princess ambazo hazikuchezwa, unasubiriwa kutoka kwa Shirikisho la Soka (TFF) kupitia Chama cha mchezo huo (TWFA), japo kanuni zinasema kuwa timu isiyoenda uwanjani bila taarifa yoyote inaweza kupoteza mechi kwa 3-0 na kupokwa pointi tano mbali na kutozwa fainali isiyopungua Sh5 milioni ambayo asilimia 50 itaenda kwa wapinzani na nyingine TFF.