Ahmed wa JKU bado anaiwaza Ligi Kuu Bara
Muktasari:
- Kipa huyo aliyemaliza msimu wa 2025-2026 akiwa na cleansheet 10, nyuma ya kinara Hamad Ubwa aliyekuwa Mlandege na cleansheet 12, amekuwa nguzo muhimu langoni akionyesha utulivu, ujasiri na uwezo wa kuokoa hatari nyingi zilizoiwezesha JKU kupata matokeo muhimu.
BAADA ya kumalizika kwa msimu wa 2025-2026 wa Ligi Kuu Zanzibar, kipa namba moja wa JKU, Ahmed Issa ameendelea kujinoa kujiandaa na msimu ujao wa 2026-2027 huku akilini mwake bado akiwa na matumaini ya kucheza Ligi Kuu Bara.
Kipa huyo aliyemaliza msimu wa 2025-2026 akiwa na cleansheet 10, nyuma ya kinara Hamad Ubwa aliyekuwa Mlandege na cleansheet 12, amekuwa nguzo muhimu langoni akionyesha utulivu, ujasiri na uwezo wa kuokoa hatari nyingi zilizoiwezesha JKU kupata matokeo muhimu.
Kutokana na kiwango chake kimewafanya wengi kumtaja kuwa miongoni mwa makipa waliokuwa na kiwango cha juu zaidi msimu huu.
Akizungumza na Mwanaspoti, kipa huyo amesema anajivunia kumaliza katika nafasi ya pili ingawaje sio katika matarajio kwani alihitaji kuwa nafasi ya kwanza.
“Nitaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza kiwango changu kwa msimu ujao na nahitaji kumaliza katika nafasi ya kwanza,” amesema.
Mbali na hilo, amesema zipo timu ambazo zinahitaji huduma yake kisiwani hapa lakini anasi JKU ndio sehemu salama kwake zaidi.
Amesema, anachotamani zaidi ni kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara, hivyo hajaona sababu ya kujiunga na timu nyingine ya Zanzibar kwani anasikilizia dili kutoka upande wa pili.