Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Woodball yatafuta viongozi wapya

WOODBALL Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na BMT Septemba 3, 2026, uchaguzi huo umepangwa kufanyika Oktoba 4, 2026 jijini Dar es Salaam, huku usaili wa wagombea ukifanyika siku moja kabla ambayo ni Oktoba 3, 2026.

BARAZA la Michezo la Taifa (BMT), limefungua rasmi mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa Tanzania Woodball Association (TWBA), huku wanachama wenye sifa wakipewa nafasi ya kuanza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wa chama hicho.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na BMT Septemba 3, 2026, uchaguzi huo umepangwa kufanyika Oktoba 4, 2026 jijini Dar es Salaam, huku usaili wa wagombea ukifanyika siku moja kabla ambayo ni Oktoba 3, 2026.

BMT ambayo ina jukumu la kusimamia na kuendeleza michezo nchini kwa kushirikiana na vyama vya michezo, imesema uchaguzi huo utasimamiwa na Kamati Maalum ya Uchaguzi ya BMT, kwa kuzingatia Katiba ya TWBA.

WOOD 01

Fomu za kuomba nafasi za uongozi zimeanza kutolewa kuanzia Septemba 3, 2026 na zinapatikana ofisi za BMT jijini Dar es Salaam, pamoja na kupitia tovuti ya BMT na mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu ni Septemba 30, 2026 saa 9:30 alasiri.

Katika uchaguzi huo, nafasi zinazotagombewa ni Mwenyekiti, Mwenyekiti Msaidizi, Katibu Mkuu, Katibu Mkuu Msaidizi na Mweka Hazina. Pia kuna nafasi za Wajumbe wa Kanda pamoja na wajumbe wa kamati mbalimbali za chama hicho.

BMT imeweka pia vigezo ambavyo mgombea anatakiwa kuwa navyo kabla ya kuingia kwenye uchaguzi.

WOOD 02

Kwa ujumla, mwombaji anatakiwa kuwa raia wa Tanzania, mwenye umri wa miaka 25 au zaidi, pamoja na kuwa na elimu isiyopungua kidato cha nne. Aidha, anatakiwa asiwe amewahi kutiwa hatiani kwa kosa la jinai na anatakiwa kuwa na uzoefu katika mchezo wa Woodball au shughuli zinazohusiana na uendeshaji wa michezo.

Kwa nafasi za juu za uongozi, ikiwemo Mwenyekiti, Mwenyekiti Msaidizi, Katibu Mkuu, Katibu Mkuu Msaidizi na Mweka Hazina, vigezo vinaenda mbele zaidi.

WOOD 03

Mgombea anatakiwa kuwa na uadilifu, haiba na hadhi ya kuiwakilisha TWBA ndani na nje ya Tanzania, huku kiwango cha elimu kinachotakiwa kikiwa si chini ya Stashahada (Diploma).

Uchaguzi huo unakuja wakati BMT ikiendelea kutekeleza jukumu lake la kusimamia, kuendeleza na kudhibiti michezo nchini kwa kushirikiana na vyama na mashirikisho ya michezo.